THE GOODNESS OF GOD

 



God has given His goodness, which is His power, to a believer who is His church to walk in victory if He will learn. That goodness is carried in the flow of the Holy Spirit in us, the Holy Spirit upon us and the Holy Spirit with us. When a person gets that goodness, blindness and ignorance is removed from him so that he can understand how things are and have the protection to enable him to walk perfectly before God.

God is not pleased with a spiritually stricken believer because he cannot be trusted with great glorious things; that is why God wants everyone to walk diligently in his vision of Love, Hope and Faith to receive his goodness. The condition for gaining all three is to live in repentance, to believe in the gospel of Jesus Christ and to have a close relationship with God; all this is enabled by the Holy Spirit. The Holy Spirit releases the gifts that work within the believer to please God and receive His love.

Swahili Translation:

SOMO: WEMA WA MUNGU

Mungu ametoa wema wake yaani nguvu zake kwa mwamini ambaye ni kanisa lake ili atembee kwa ushindi kama atajifunza. Wema huo unabebwa katika mtembeo wa Roho Mtakatifu ndani yetu, Roho Mtakatifu juu yetu na Roho Mtakatifu pamoja nasi. Mtu akipata wema huo anaondolewa upofu na ujinga ili afahamu mambo yalivyo na apate ulinzi wa kumwezesha kutembea kwa ukamilifu mbele za Mungu.

Mungu hapendezwi na mwamini aliyedumaa kiroho kwa sababu hawezi kuaminiwa kwa mambo makubwa yenye utukufu; ndio maana Mungu anamtaka kila mtu atembee kwa bidii katika dira yake ya Upendo, Tumaini na Imani ili apokee wema wake. Sharti la kupata mambo hayo matatu ni kuishi kwa toba, kuiamini injili ya Yesu Kristo na kuwa na uhusiano wa karibu na Mungu; haya yote huwezeshwa na Roho Mtakatifu. Huyo Roho Mtakatifu huachilia vipawa na karama zinazotenda kazi ndani ya mwamini ili ampendeze Mungu na apokee upendo wake.

 By Servant of God Apostle and Prophet Josephat Elias Mwingira, Efatha Church.  

Comments