PEOPLE WHO KNOW THEIR DREAMS ARE ALWAYS IN PAIN.

 


Dreamers have a lot of obstacles from their opponents. Before seeing your dream come true there is a lot of pain, because DREAM is like a baby coming out of the mother's womb. Don't worry about going through pain to achieve your dream because you are on the right Path.

Joseph went through a lot of pain before achieving his dream; he was sold, imprisoned but ended up being a very great man and became a help to his brothers. Jesus before achieving His dream He went through the cross and was nailed, but now HE is the LORD OF LORDS and reigns over all the earth. Child of God do not give up, fight for your dream until it is fulfilled.

Swahili Translation

WATU WANAOJUA NDOTO ZAO MARA ZOTE WAPO KATIKA MAUMIVU.

Wabeba ndoto wana vizuizi vingi sana kutoka kwa wapinzani wao. Kabla ya kuona ndoto yako ikitimia kuna maumivu mengi; kwa sababu NDOTO ni kama mtoto akitoka katika tumbo la mama yake. Usiwe na mashaka unapopitia maumivu ili kuifikia ndoto yako kwa sababu upo katika Njia sahihi.

Kabla ya Yusufu kuifikia ndoto yake, alipita kunako maumivu mengi; aliuzwa, alifungwa gerezani lakini aliishia kuwa mtu mkuu sana na akawa msaada kwa ndugu zake. Yesu kabla ya kuifikia ndoto yake, alipitia msalaba na akapigwa misumari; lakini sasa YEYE ni BWANA wa MABWANA na anatawala dunia nzima. Mwana wa Mungu usikate tamaa, pigania ndoto yako mpaka itimie.

By Servant of God Apostle and Prophet Josephat Elias Mwingira, Efatha Church.

Comments