KNOW THE WEAPONS OF DEVIL WHICH CAN DESTROY YOU AND MAKE YOU FAIL TO REACH YOUR GREATNESS

 


It is true that you want to be victorious in your life, but for you to get that victory you must know fist what will make you fail when you start your journey. Devil uses the following things to make sure that you end up on the way:

  • Confusion: confusion is very dangerous for you because it makes you feel inferior, it is there to devalue you so that you feel worthless and that there is nothing worthwhile you can do. Always a mango tree cannot produce oranges, now if you feel worthless, you are nothing, you can do nothing and you are weak you will never be able to do anything powerful in your life.
  • Oppression: Whenever you want to do something you feel tired. Every time you want to do something for you to go somewhere in life you find yourself tired and say I will do it tomorrow. The devil's purpose in using oppression is to make you stop and end up on the road.
  • Temptations: the devil will use any kind of influence to get you out of the purpose.
  • Lies / deceptions: he will bring issues of deception to you, why deception? Because he wants to get you out of line. He knows when you get to where you are intended you will help many and you will be a great person, so he will bring you trials to get you out of purpose.

Many people have changed their purpose because of deception. You find a person wanted to be a doctor but someone can come and tell him, there are too many doctors and if you study medicine you will have problem in finding a job so you better pursue this. You should realize that the thing that will make you a great person is not easy; anything difficult is your success, something simple does not make you a great person. If you read the Bible you will see that no one was great by doing simple things.

The path to your GREATNESS is not easy so be prepared for your greatness. Deception will come to get you out of your square so you have to be careful.

Swahili Translation:

TAMBUA SILAHA ZA IBILISI AMBAZO ZINAWEZA KUKUANGUSHA ILI USIWEZE KUFIKIA UKUU WAKO.

Ni kweli unataka kuwa mshindi katika maisha yako lakini ili uweze kufikia huo ushindi inakupasa utambue kwanza kipi kitakacho kufanya ushindwe pale unapo ianza safari yako. Ibilisi anatumia mambo yafuatayo ili kuhakikisha wewe unaishia njiani:

  • Bumbuwazi: bumbuwazi ni hatari sana kwako kwa sababu linakufanya ujione wewe ni mdogo, lipo ili kukushusha thamani ili ujione kuwa hauna thamani na kwamba hakuna cha thamani unachoweza kukifanya; siku zote mti wa muembe hauwezi kuzaa machungwa, sasa kama unajiona kuwa hauna thamani, wewe si kitu, hauwezi chochote na wewe ni dhaifu kamwe hautaweza kufanya kitu chenye nguvu katika maisha yako.
  • Mkandamizo: Mara zote unapotamani kufanya jambo unaona uchovu. Wakati wote ambao unatamani kufanya kitu ili usogee mahali fulani ki maisha unajikuta umechoka unasema nitafanya kesho, lengo la ibilisi kutumia mkandamizo ni ili uache yaani uishie njiani.  
  • Majaribu: ibilisi atatumia ushawishi wa aina yeyote ili kukuondoa kwenye kusudi.
  • Uongo/udanganyifu: ataleta jambo la udanganyifu kwako, kwa nini udanganyifu? Kwa sababu anataka kukuondoa kwenye mstari, anajua ukifika kule uliko kusudiwa utawasaidia wengi na utakuwa mtu mkuu, hivyo atakuletea majaribu ili kukutoa kwenye kusudi.

Watu wengi wamebadilishia kusudi lao kwa sababu tu ya udanganyifu, unakuta mtu alitaka kuwa daktari lakini anaweza kuja mtu na kumwambia, madakari wako wengi sana na ukisomea udaktari utapata shida ya ajira hivyo ni afadhali usomee hiki; unapaswa kutambua kuwa kitu kitakacho kufanya wewe kuwa mtu mkuu siyo chepesi, kitu chochote kitakacho kupa ugumu ndio kilicho na mafanikio yako, kitu rahisi hakikupi wewe kuwa mtu mkuu. Ukisoma katika Biblia utaona hakuna yeyote aliyekuwa mkuu kwa kufanya mambo rahisi.

Njia ya kuelekea UKUU wako siyo nyepesi hivyo jiandae kwa ukuu wako. Udanganyifu utakuja ili kukuondoa kunako mraba wako hivyo yakupasa wewe kuwa makini.

By Servant of God Apostle and Prophet Josephat Elias Mwingira, Efatha Church.

Comments