THE ENEMY OF YOUR BLESSINGS


The enemy of your blessings is the older spiritual brother, the devil. The enemy of the blessed is the character of an older spiritual brother, the devil. Darkness first existed in this world before Light that is why devil is called an older brother. The book of Genesis 1: 1-4 says God created heaven and earth and the earth was without form, and void; that is, blessings do not come from the land but one can only find success, because the older brother is the enemy of the blessing.

The older brother opposes the greatness of man. If you listen to the older brother you will not be safe, you must encounter shameful things because he has a tendency of taking away anything that will give you your greatness. When that spirit deals with your life you will see attacks and oppression. (Genesis 31: 40- 42)

The behavior of the older brother has a lot of tricks, when you have a vision for tomorrow he must come to cause you to fail. For example:  If you want to start a business he will persuade you to work together. If you give him your money to start the business he leaves with them and if you ask him he will not answer you. You find yourself looking for another capital and you will never find it.

When you see a conflict between you and your partner whether in business or between husband and wife and you do not understand what is happening know that is not a physical battle but a spiritual one. The older brother is at work and you have to know what to do. (Genesis 25: 21 - 23)

Swahili Translation:

ADUI WA BARAKA ZAKO.

Adui wa baraka zako ni kaka mkubwa wa kiroho yaani shetani. Adui wa mbarikiwa ni tabia aliyonayo kaka mkubwa wa kiroho yaani shetani. Giza lilitangulia kuwepo katika dunia hii kabla ya Nuru ndio maana shetani huitwa kama mkubwa. Kitabu cha Mwanzo 1: 1-4, kinasema Mungu aliziumba mbingu na nchi nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu; yaani baraka hazitoki katika nchi bali mtu anaweza kupata mafanikio tu, kwa sababu kaka mkubwa ni adui wa baraka.

Kaka mkubwa hupingana na ukuu wa mtu. Ukimsikiliza kaka mkubwa hutakuwa salama, ni lazima upatikane na mambo ya aibu kwa sababu anatabia ya kuondoa chochote kitakachokupa ukuu wako. Hiyo roho inaposhughulika na maisha yako utaona mashambulizi na hali ya kudhulumiwa. (Mwanzo 31:40 - 42).

Tabia ya kaka mkubwa ina hila nyingi, unapokuwa na maono ya kesho ni lazima atakuja kukusababisha ushindwe. Kwa mfano. Kama unataka kuanzisha biashara atakushawishi ili mfanye pamoja. Ukimpa pesa zako ili kuanza hiyo biashara anaondoka nazo na ukimuuliza hatakujibu. Unajikuta ukitafuta mtaji mwingine na kamwe hutapata.

Unapoona kuna mapambano kati yako na mwenzako iwe katika biashara au kati ya mume na mke na huelewi yanakotokea fahamu hiyo siyo vita ya kimwili bali ni ya kiroho. Kaka mkubwa yupo kazini na ni lazima ujue jambo la kufanya. (Mwanzo 25: 21 - 23)

By Servant of God Apostle and Prophet Josephat Elias Mwingira, Efatha Church.

Comments