THINK BEFORE YOU ACT




Most people like to do things to be celebrated by people but few of those who celebrate think about the consequences of what happened. The result of something is what determines the intention of the action whether it was good or bad. When you first weigh the consequences of your actions, that is wisdom. God looks at a person's intent to do something and not what he did.

The way to stop making mistakes is to think first about the consequences of everything you want to do. When you do something without understanding it you run the risk of losing it yourself. If you do not understand something well before you do, take time to think and ask those who know so that you do not fall into remorse.

Example; When you go to the shop do not collect the product first before you know what you want to buy and its prices. Only a fool would choose a product before knowing the price. When you think before you act, it helps you not to make repeated mistakes and that is the healing of actions.

Ephesians 5: 15 -17 “See then that you walk [a]circumspectly, not as fools but as wise, 16 redeeming the time, because the days are evil. 17 Therefore do not be unwise, but understand what the will of the Lord is.”

God loves us but when He sees our evil deeds He become angry with us because those evil things make us unclean before Him. A born-again is changed inside and that is the true gospel.

2 Corinthians 5: 17 “Therefore, if anyone is in Christ, he is a new creation; old things have passed away; behold, all things have become new.”

If we are careful in our thinking before we act, even the devil will not be able to play with us.

Swahili Translation:

Watu wengi hupenda kufanya mambo ili washangiliwe na watu lakini ni washangiliaji wachache hutafakari juu ya matokeo ya jambo lililofanyika. Matokeo ya jambo ndiyo hubainisha dhamira ya tendo kama lilikuwa jema au baya. Unapopima kwanza matokeo ya jambo unalotaka kufanya, hiyo ni hekima. Mungu huangalia dhamira ya mtu katika kufanya jambo na si kile alichofanya.

Namna ya kuacha makosa ni kufikiri kwanza matokeo ya kila unachotaka kufanya. Unapofanya jambo bila kuelewa unajiingiza katika hatari itakayo kumaliza mwenyewe. Kama huelewi jambo vizuri kabla ya kufanya, chukua muda kufikiri na uliza wanaojua ili usiingie katika majuto.

Kwa mfano; Unapokwenda dukani usikusanye bidhaa kwanza kabla ya kujua unataka kununua nini na bei zake. Ni mjinga tu ndiye huchagua bidhaa kabla ya kujua bei. Unapofikiri kabla ya kutenda, hukusaidia kutokosea mara kwa mara na huo ndio uponyaji wa matendo.

Waefeso 5: 15 -17 "Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima; mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu. Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana."

Mungu anatupenda ila anapoona matendo yetu maovu huchukizwa nasi kwa kuwa maovu hayo hutufanya wachafu mbele zake. Aliyezaliwa mara ya pili amebadilika ndani yake na hiyo ndiyo injili ya kweli.

2 Wakorintho 5:17 " Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya."

Tukiwa makini katika kufikiri kabla ya kutenda hata shetani hataweza kutuchezea kamwe.

By Servant of God Apostle and Prophet Josephat Elias Mwingira, Efatha Church.

Comments