SALVATION




Salvation is important to everyone because it carries redemption and healing. When a person accepts Jesus as Lord and Savior of his life, the essence of the pain of his heart is redeemed.
The origin of the diseases is removed from him and transferred from their lineage to the lineage of Abraham who is our father of Faith. At this point, blessings must follow him.

He has to admit that he no longer needs to be followed by the past because his ways are new. He needs the eyes of the spirit which is the understanding to see again. Therefore, he should no longer be on the wrong path. Salvation is essential for anyone who wants to succeed in God. It is a tool that carries redemption and healing.

In salvation there is worship of the true God, Faith in the true God who made heaven and earth, Man's blessings from God, the deliverance of man from the kingdom of darkness, gifts of the Holy Spirit and gifts of God, the eternal life and many more.

Swahili Translation:

Wokovu ni muhimu kwa kila mtu maana hubeba ukombozi na uponyaji, mtu anapompokea Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yake, kiini cha maumivu ya moyo wake hukombolewa. Asili ya magonjwa huondolewa kwake na kuhamishwa toka kwenye ukoo wao kwenda kwenye ukoo wa Ibrahimu ambaye ni baba yetu wa Imani. Akifikia hatua hii, baraka lazima zimfuate.

Anatakiwa kukiri kuwa hahitaji tena kufuatwa na mambo ya kale kwa kuwa njia zake ni mpya. Anahitaji macho ya roho ambayo ni ufahamu ili aone tena. Anavyoendelea kupata mafundisho na kuelewa Neno, hupata ufahamu. Hivyo basi, hapaswi tena kuwa kwenye njia zisizofaa. Wokovu ni muhimu kwa mtu yeyote anayetaka kufanikiwa katika Mungu. Ni chombo kinachobeba ukombozi na Uponyaji.

Ndani ya wokovu kuna Ibada kwa Mungu wa kweli, Imani ya kumwamini Mungu wa kweli aliyeumba mbingu na nchi, Baraka za mtu kutoka kwa Mungu, ukombozi wa mtu kutoka ufalme wa giza, vipawa vya Roho Mtakatifu na karama za Mungu, kupata uzima wa milele na mengine mengi.

By Servant of God Apostle and Prophet Josephat Elias Mwingira, Efatha Church.

Comments