RESPECT WHAT YOU ARE GIVEN BY GOD BECAUSE IT’S WHAT YOU DESERVE




Many people get many things from God directly or by being laid hands by the servants of God but they do not appreciate them. Ask yourself if you were the giver of those gifts and then saw that those who you give them gifts don’t appreciative them, how would you feel?

Example; You have been given the opportunity to be a pastor and then you don’t value that position, what do you think does the one who gave you that opportunity sees? Likewise, deliverance and healing cannot occur in a person's life if he does not know his value.

The cost of the deliverance of the children of Israel was the time of their journey from Egypt to Canaan but they did not appreciate it and died in the wilderness. So it is even now, God has saved you from the powers of darkness but because of not knowing its value, you will live without seeing the joy of your salvation.

Respect what God gives you, because that's what you deserve. Don't look at your own wants based on your desires, for they will give you pain.

Swahili Translation:

HESHIMU UNACHOPEWA NA MUNGU MAANA NDIYO STAHILI YAKO

Watua wengi hupata vitu vingi kutoka kwa Mungu moja kwa moja au kupitia kuwekewa mikono na watumishi lakini hawavithamini. Jiulize kama ungekuwa mtoa hizo zawadi alafu unaona unaowazawadia hawazithamini ungejisikia je?

Kwa mfano; Umepewa nafasi ya kuwa Mchungaji wa kituo halafu huthamini hiyo nafasi. Je unafikiri yule aliyekupa anaona je? Vivyo hivyo, ukombozi na uponyaji hauwezi kutokea kwenye maisha ya mtu kama hajui uthamani wake.

Gharama ya ukombozi wa wana wa Israel ilikuwa ni muda wa safari yao kutoka Misri kwenda Kaanani lakini hawakuthamini hilo wakafia jangwani. Ndivyo ilivyo hata sasa, kama Mungu amekuokoa kutoka kwenye nguvu za giza lakini kwa sababu ya kutojua uthamani wake, utaishi bila kuona furaha ya wokovu wako.

Heshimu Mungu anachokupa, maana ndicho unachostahili. Usiangalie matakwa yako yanayotokana na tamaa zako, maana yatakupa maumivu.

By Servant of God Apostle and Prophet Josephat Elias Mwingira, Efatha Church.

Comments