KNOW WHAT YOU ARE SUPPOSED TO DO




When you have understanding, and know what you are supposed to do, you will prevent all kind of destruction intended for you. One day the Lord Jesus and His disciples, as they sailed from Tiberius to the other side, fell asleep, wind and storm began to blow and the vessel was about to sink. His disciples were terrified because they did not have faith; they went to awaken the Lord Jesus and He told them; "Shut up, why do you have so little faith?" Then he rebuked the storm and it calmed down.

If you do not question yourself you will not know yourself but you will live without direction and will remain in trouble; but daily self-examination allows you to follow instructions. When the prodigal son decided in his heart and know that he was lost, he decided to return to his father's house because there was plenty while he lived in misery and hopelessness.

When you examine yourself you see if you have done good or bad, and the following happens: -
  • You save yourself from destruction
  • You heal your environment easily without using too much force
  • You see the healing power at work in you to help other people who are suffering
  • People begin to rejoice and glorify God for you because you have done well
ANNOUNCEMENT:

Know what you must do for destruction and doubt to stay away from you, In Jesus' Name.

Swahili Translation:

SOMO: FAHAMU UNACHOTAKIWA KUFANYA.

Ukiwa na Ufahamu na kujua unachotakiwa kutenda, utazuia kila aina ya uharibifu uliokusudiwa kwako. Siku moja Bwana Yesu na wanafunzi wake, wakiwa wanasafiri kwa merikebu kutoka Tiberia kwenda upande mwingine alilala. Upepo na dhoruba ulianza kuvuma na chombo kikataka kuzama. Wanafunzi wake waliingiwa na hofu kwa sababu wote hawakuwa na imani; walienda kumwamsha Bwana Yesu naye aliwaambia; "tulieni mbona mna imani haba?" Ndipo akakemea dhoruba nayo ikatulia.

Usipojihoji huwezi kujitambua bali utaishi bila mwelekeo na kubaki na matatizo; lakini kujihoji kila siku hukuwezesha kufuata maagizo. Mwana mpotevu alipoazimia moyoni mwake akajua yakuwa amepotea, aliamua kurudi nyumbani kwa baba yake kwani kulikuwa na utele wakati yeye anaishi kwa taabu pasipo matumaini.

Unapojihoji unaona kama umefanya mema au mabaya, na yafuatayo hutokea:-
  • Unajiponya kutoka kwenye uharibifu
  • Unaponya mazingira yako kirahisi bila kutumia nguvu nyingi
  •  Unaona nguvu ya uponyaji ikifanya kazi ndani yako ili kusaidia watu wengine wanaoteseka
  • Watu huanza kumshangilia na kumtukuza Mungu kwa ajili yako kwa sababu umefanya vizuri
TANGAZO:

Fahamu unachotakiwa kufanya ili uharibifu na mashaka vikae mbali nawe, Katika Jina la Yesu.

By Servant of God Apostle and Prophet Josephat Elias Mwingira, Efatha Church.

Comments