BLESSING




Blessings are for the faithful and the perfect; to satisfy their needs and not their wants. Without Blessing people perish but the blessed is satisfied with what he has, either all those who want to be satisfied with Him get their needs. He is not bankrupt and cannot be bankrupt unless God approves for his own reasons. Although no one is born perfect but it is up to the individual to be perfect. The Word says that Jesus was perfect and pleased God and men.

Blessings are neither success nor money; but when a man has blessing, money comes by itself. Blessings are always good but success and money can be good or bad. When some people are successful, they live with anxiety and even seek protection because they have many enemies. His enemies may be his chief of staff, people in his workplace or business and his closest relatives. All of these can destroy what he has. For example; Samson was successful, but not blessed that is why he was destroyed easily.

The blessed one does not need to fight for himself, but God Himself fights for and protects him. When a person crosses from success to prosperity it is not easy to be destroyed because he is surrounded by God's protection. To achieve this, we must renounce worldly pleasures and please God first. Live as God's Word says, then the devil will not even touch your body.

Romans 12:1 says, “I beseech you therefore, brethren, by the mercies of God, that you present your bodies a living sacrifice, holy, acceptable to God, which is your reasonable service.”

It's better to reach a point of success than poverty.

Swahili Translation:

Baraka ni kwa waaminifu na wakamilifu; ili kutosheleza mahitaji yao na sio matakwa yao. Pasipo Baraka watu huangamia lakini aliyebarikiwa hutoshelezwa na alichonacho aidha wote wanaotaka kutoshelezwa naye hupata mahitaji yao. Hafilisiki wala hawezi kufilisiwa labda Mungu atoe kibali kwa sababu zake mwenyewe. Ingawa hakuna mtu aliyezaliwa mkamilifu lakini ni juu ya mtu mwenyewe kuwa mkamilifu. Neno linasema Yesu alikuwa mkamilifu akimpendeza Mungu na wanadamu.

Baraka sio mafanikio wala fedha; bali mtu akiwa na Baraka fedha huja yenyewe. Baraka daima ni njema lakini mafanikio na fedha huweza kuwa mazuri au mabaya. Baadhi ya watu wanapopata mafanikio huishi kwa wasiwasi hata kutafuta ulinzi kwa maana anamaadui wengi. Adui zake wanaweza kuwa mkuu wake kazini, watu walio katika eneo lake la kazi au biashara, ndugu na jamaa zake wa karibu. Wote hawa wanaweza kuharibu na kuangamiza alivyonavyo. Kwa mfano; Samsoni alikuwa na mafanikio lakini sio Baraka ndiyo maana aliangamizwa kwa urahisi.

Aliyebarikiwa hahitaji kujipigania mwenyewe, bali Mungu mwenyewe humpigania na kumlinda. Mtu akivuka kutoka kwenye mafanikio na kwenda ustawi siyo rahisi kuangamizwa kwa maana anazungukwa na ulinzi wa Mungu. Ili kufikia hatua hii, ni lazima kuacha mambo ya dunia ya kuufurahisha mwili na ampendeze Mungu kwanza. Ishi kama Neno la Mungu linavyosema, ndipo shetani hata gusa mwili wako.

Warumi 12:1 inasema, “Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana”.

Ni vema kufikia hatua ya mafanikio kuliko umaskini.

By Servant of God Apostle and Prophet Josephat Elias Mwingira, Efatha Church.

Comments