BLESSING




God has set a standard for success and prosperity. The process is in three stages where He begins to prohibit things that we should not do and what we should do and the consequences. A person who delights in the law of the Lord will succeed, prosper and be blessed because God says everything he does will prosper.

He will be like a tree planted by streams of water, whose leaves never wither and bear fruit in his season without ending (Psalm 1:2). Bearing fruit in his season means there is a waiting time to get fruits. Those who know God should understand that they should wait to receive from Him because they delight in His law.

God told Joshua that wherever his foot shall step He has given him, but he should be strong and courageous. He warned him before because when God's people go to their blessings there are many obstacles which hinder them to be as they how they are purposed. This is not the case with people of this world because they have their own way of success. They can sacrifice their close relatives fearlessly in order to be rich and gain wealth. They have been written in the bible that they sacrificed their sons and daughters unto devils (Psalm 106: 37).

The important thing for a person who wants to prosper is to learn more about God and submit unto Him. When he did that, the King desires her beauty, it’s like women who knows how to submit to their husbands receives favour (Psalm 45:11-12). God becomes your giver and lastly prosperity becomes very easy, otherwise you cannot prosper through your own power without favour from God.

Job lost everything but he submitted himself unto God and at the end God was pleased with him. He commanded all things to follow him and he became rich more than before. That is why it is not right to despise a person who has nothing today because when that person shows himself before God that he can be trusted, God will bless him because He is the one who has the fate of his blessings.

Swahili Translation: 

SOMO: BARAKA

Mungu ameweka utaratibu wa kufuatwa ili kupata mafanikio na ustawi. Utaratibu huo uko katika hatua tatu ambapo anaanza na kukataza mambo ambayo hatupaswi kufanya yale ya kufanya na matokeo yake. Mtu ambaye anapendezwa na sheria ya Bwana atafanikiwa, atastawi na kubarikiwa kwa sababu Mungu anasema kila alitendalo litafanikiwa.

Atakuwa kama mti uliopandwa kando ya vijito vya maji, ambao wakati wote majani yake hayanyauki na huzaa matunda kwa wakati bila kukoma (Zaburi 1:2). Kuzaa matunda kwa majira yake inamaanisha kuna kipindi cha kusubiri na kupata matunda. Watu wanaomjua Mungu wanapaswa kufahamu kuwa wanatakiwa kusubiri kupokea kutoka kwake kwa sababu wanapendezwa na sheria yake.

Mungu alimwambia Yoshua kuwa popote atakapokanyaga kwa miguu yake amempa, lakini awe hodari na moyo wa ushujaa. Alimtahadharisha kabla kwa sababu watu wa Mungu wanapoendea nafasi zao za baraka kuna vikwazo vingi vya kuwazuia wasiwe kama walivyokusudiwa. Sivyo ilivyo kwa watu wa dunia hii kwa sababu wao wanazo njia zao za kufanikiwa. Wanaweza kutoa kafara za watu wao wa karibu bila hofu ili wapate mali na utajiri. Habari zao zimeandikwa katika biblia kuwa waliwatoa wana wao na binti zao kuwa dhabihu kwa mashetani ( Zaburi 106 : 37)

Mtu anayetaka kustawi jambo la muhimu ni kujifunza zaidi kuhusu Mungu na kujitiisha kwake. Anapofanya hivyo mfalme anautamani uzuri wake, ni kama wanawake wahudumu wanaojua kujitiisha kwa Bwana zao hupata kibali. Zaburi 45:11-12) Mungu anakuwa mpaji wako na mwishoni unastawi kwa urahisi sana, vinginevyo huwezi kustawi kupitia nguvu zako pasipo kupata kibali kwa Mungu.

Ayubu alipoteza kila kitu lakini alijitiisha kwa Mungu na mwishowe alimfurahia. Aliamuru vitu vimjilie, akawa tajiri zaidi ya alivyokuwa mwanzo. Ndio maana sio vema kumdharau mtu asiye na kitu leo kwani akijionesha kwa Mungu kuwa anaweza kuaminika; Mungu humbariki kwa sababu ndiye aliye na hatma ya baraka zake.

By Servant of God Apostle and Prophet Josephat Elias Mwingira, Efatha Church.

Comments