WITH HOPE, YOU ARE BLESSED




Psalm 1:1 “Blessed is the man Who walks not in the counsel of the [a]ungodly, Nor stands in the path of sinners, Nor sits in the seat of the scornful;”

Why God call this person blessed? It is because this person has an expectation that is hope and no one can take it away; no one can take away your Hope because that Hope is created by God in you and not man.

God created you with Hope that is why He calls you blessed, why? Because you have expectation in you. No one was created with money, housing, clothes or education, no one was born a king or doctor nor was anyone born rich but each of us was created with hope in him so that whatever he is hoping would come to him.

Nobody is born a failure in the world but our failure is due to the environment we were born, many of us have found ourselves in failure, but you should know that environment is what made you fail and not how you were created, creation made us hopeful to win.

We were created to create. God still has hopes in you and He is not tired, that is why even today He saves people. He hopes that one day you too will be saved and return to your hope and be able to win.

Don't look at your appearance, the education you have or the family you came from but look at the one who created you and the HOPE you have so you can be a WINNER here on earth.

Swahili Translation:

Zaburi 1:1 “Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.”

Ni kwa nini Mungu anamuita mtu huyu heri? Ni kwa sababu mtu huyu anamatarajio yaani tumaini na hakuna anayeweza kuliondoa; hakuna anayeweza kuondoa Tumaini lako kwa sababu hilo Tumaini limeumbwa na Mungu ndani yako na si mwanadamu.

Mungu alikuumba wewe pamoja na Tumaini ndiyo maana anakuita wewe heri, kwa nini? Kwa sababu unalo tarajio ndani yako. Hakuna mtu hata mmoja aliumbwa akiwa na fedha, nyumba kubwa, nguo wala elimu, hakuna aliyezaliwa akiwa mfalme au Daktari wala hakuna mtu aliyezaliwa akiwa tajiri bali kila mmoja wetu aliumbwa akiwa na Tumaini ndani yake ili chochote anacho kitumaini kipate kumjilia.

Hakuna mtu aliyezaliwa kama wa kushindwa huku duniani lakini kushindwa kwetu kunatokana na mazingira tuliyozaliwa, wengi wetu tumejikuta tumeshindwa, lakini unapaswa kujua kuwa mazingira ndiyo yamekufanya ushindwe na siyo uumbaji, uumbaji ulitufanya sisi tuwe na Tumaini ili tupate kushinda.

Tuliumbwa ili tuumbe, Mungu bado anatumaini na wewe hajachoka na ndiyo maana hata leo anaokoa, anamatumaini kwamba siku moja na wewe utaokoka ili ulirudie tumaini lako ili uweze kushinda.

Usiangalie sura yako, elimu uliyonayo wala familia uliyotoka bali muangalie yule aliyekuumba na lile TUMAINI ulilonalo ili uweze kuwa MSHINDI huku duniani.

By Servant of God Apostle and Prophet Josephat Elias Mwingira, Efatha Church.

Comments