THE SPIRIT OF KNOWLEDGE




The knowledge of God brings creativity that ease the performing of unique works with good quality and standards to bring about a better life. The Spirit of Knowledge works with the diligent and allows no one to rest until something happens in order to enrich and prosper him. This Spirit enables a person to learn something in a short period of time and become a champion and even design projects that generate employment for others.

When the Spirit of Knowledge comes to you, you cannot become poor for it draws empowerment to your advantage and there is no failure as there is He who empowers you. It draws on implementation requirements for you to achieve prosperity.

Ephesians 3:20 “Now unto him that is able to do exceeding abundantly above all that we ask or think, according to the power that worketh in us”

Even when you lack the power of God, this Spirit empowers you to win. It brings you from down and takes you to a higher level; it allows you to work hard so that you do not become inferior and prosper within a short period of time and amaze people.

Mark 10:31 “But many that are first shall be last; and the last first.”

Swahili Translation:

Maarifa ya Mungu huleta ubunifu unaoleta wepesi na urahisi wa kutenda kazi za kipekee, zenye ubora na viwango ili kuleta maisha mazuri. Roho wa Maarifa hufanya kazi na walio na bidii na hamruhusu mtu kupumzika hadi jambo litendeke, ili kumtajirisha na kumstawisha, humwezesha mtu kujifunza kwa muda mfupi hata kuwa bingwa kiutendaji na hata kubuni miradi ambayo huzalisha ajira kwa wengine. Nguvu hii ikikosekana kwa mtu hawezi kustawi wala kumudu maisha, anaishia kuwa na madeni na kutawanya hata kidogo alichonacho.

Roho wa Maarifa akishaingia ndani yako huwezi kuwa maskini, kwani huvuta uwezesho wa kukufanikisha na hakuna kushindwa kwani yuko akuwezeshaye. Huvuta mahitaji ya utekelezaji ili ukamilishe kustawi.

Waefeso 3:20 “Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu.”

Hata kama umepungukiwa uweza wa Mungu unajaziliza, upate kushinda. Inakutoa chini na kukupeleka daraja la juu; inakuwezesha kuwa na bidii ya kazi ili usiwe mtu duni na ndani ya muda mfupi unastawi hadi kushangaza watu.

Marko 10:31 “Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho; na wa mwisho watakuwa wa kwanza”


By Servant of God Apostle and Prophet Josephat Elias Mwingira, Efatha Church.


Comments