STAY AWAY FROM SIN




Child of God, honour God’s plan and purpose in your life for you to succeed. The hardship and pain are allowed in your life because of SIN. Sin caused suffering and pain in all aspects of human life from the beginning.

Genesis 3:16, 18 “Unto the woman he said, I will greatly multiply thy sorrow and thy conception; in sorrow thou shalt bring forth children; and thy desire shall be to thy husband, and he shall rule over thee. 18 Thorns also and thistles shall it bring forth to thee; and thou shalt eat the herb of the field;”

Even now there are people who are saved but living a difficult life because they do not follow the instructions. Do not let your personality be bought because of the distress you have or the desire of the eyes and do not let the need or trouble lead you to sin. The bible says LET YOUR REQUEST BE KNOWN UNTO GOD and not people. Desire to do what God has commanded through His Word, listen to the teachings of God's people for you to see your destiny which was purposed before your birth, for it is God who has prepared that day.

Genesis 4:7 “If thou doest well, shalt thou not be accepted? and if thou doest not well, sin lieth at the door. And unto thee shall be his desire, and thou shalt rule over him.”

Sin is invisible to the eyes of the flesh even when it strikes a person, but we see its consequences.
Sin existed before we existed and troubles every born of a woman and it is always its desire to win a person through influence.
You should know that good and evil work together in a person, so it's important to look at what you do.

Don't let sinners persuade you but go by following the Word to overcome sin by obeying the commandments, which God commands through His servants to attain your glory

Proverb 1:10 “My son, if sinners entice thee, consent thou not.”

John 10:9 “I am the door: by me if any man enter in, he shall be saved, and shall go in and out, and find pasture.”

Sin blinds the eyes of man to see the door of his good, God has prepared a way for every saved person to come to the gate (JESUS) to find his destiny, but sin is waiting for him at the door to stop him because that is where God has prepared the table before his enemies. If you choose to stay away from sin and things that displease God you will not suffer from demons, diseases or poverty.

Swahili Translation:

KAA MBALI NA DHAMBI.

Mwana wa Mungu heshimu ratiba na mpango wa Mungu katika maisha yako ili ufanikiwe, magumu, machungu na maumivu vinaruhusiwa kwako kwa sababu ya DHAMBI. Dhambi ilisababisha magumu na maumivu kwenye nyanja zote za maisha ya mwanadamu toka mwanzo.

Mwanzo 3:16,18Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala. Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako; michongoma na miiba itakuzalia, nawe utakula mboga za kondeni;"

Hata sasa kuna watu waliookoka lakini wanaishi maisha magumu kwa sababu hawafuati utaratibu. Usikubali utu wako ununuliwe kwa sababu ya dhiki uliyonayo au tamaa ya macho wala usiruhusu uitaji au shida ikupeleke kwenye kufanya dhambi. Biblia inasema, HAJA ZAKO NA ZIJULIKANE NA BWANA na sio zijulikane na mtu. Tamani kufanya yale ambayo Mungu ameagiza kupitia Neno lake, sikiliza mafundisho ya watu wa Mungu upate kuiona siku yako iliyokusudiwa kabla ya kuzaliwa kwako, maana ni Mungu ndiye aliyeiandaa hiyo siku.

Mwanzo 4:7 “Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde?"

Dhambi haionekani kwa macho ya nyama japokuwa inamwotea mtu, bali tunaona matokeo yake. Dhambi ilikuwepo kabla ya sisi kuwepo na inamtumikisha kila aliyezaliwa na mwanamke tena daima inatabia ya kuotea mtu ili imteke kupitia ushawishi. Fahamu kuwa wema na uovu unafanya kazi pamoja ndani ya mtu, hivyo ni muhimu kuangalia unachofanya.

Usikubali wenye dhambi wakushawishi bali nenda kwa kufuata Neno ili ushinde dhambi kwa kutii maagizo, unayoagizwa na Mungu kupitia watumishi wake ili ufikie utukufu wako.

Mithali 1:10 “Mwanangu , wenye dhambi wakikushawishi, Wewe usikubali”

Yohana 10:9 “Mimi ndimi mlango; mtu akiingia kwa mimi, ataokoka; ataingia na kutoka, naye atapata malisho".

Dhambi inapofusha macho ya mtu asiweze kuona mlango wa mema yake, kila mtu aliyeokoka Mungu amemwandalia njia ya kufika langoni (YESU), ili apate aliyokusudiwa, bali dhambi ipo inamsubiri mlangoni ili kumzuia kwa kuwa hapo ndipo Mungu amemwandalia meza mbele za adui zake. Ukiamua kukaa mbali na dhambi na Mambo yasiyompendeza Mungu hutasumbuliwa na mapepo, magonjwa wala umaskini.

By Servant of God Apostle and Prophet Josephat Elias Mwingira, Efatha Church.

Comments