OBEY GOD'S INSTRUCTIONS




You who are saved by God, stay away from DEFILEMENT and make sure you live a HOLY life for the Spirit of the Lord to be with you. For you to be happy with life in Christ, obey the instructions from God.

Isaiah 1: 19  “If you are willing and obedient, You shall eat the good of the land;”

In doing the work of God, be ready to be sent without debate, and don't allow questions in your mind.

Isaiah 6: 8-9 “Also I heard the voice of the Lord, saying: “Whom shall I send, And who will go for Us?” Then I said, “Here am I! Send me.” And He said, “Go, and tell this people: ‘Keep on hearing, but do not understand; Keep on seeing, but do not perceive.”

If you are not ready to be sent, you will never hear the voice of the Lord or see the miracles of God and you will never understand because you are stubborn.

You might be fasting so much but nothing happens in your life because you don’t follow instructions. Follow the instructions because there is a reward. Learn to be gentle and generous and never rush to make your decisions. Learn how to listen to the Holy Spirit.

Numbers 12:3 “Now the man Moses was very humble, more than all men who were on the face of the earth.”

Do good to others and do not seek revenge, also keep and control your mouth. Speak good to yourself and others.

Ecclesiastes 6: 6- 7  even if he lives a thousand years twice—but has not seen goodness. Do not all go to one place? All the labor of man is for his mouth, And yet the soul is not satisfied.”

Desire to be in the house of the Lord where there is God’s presence all the time as David did and let that be your character.

Psalm 27: 4 “One thing I have desired of the Lord, That will I seek: That I may dwell in the house of the Lord All the days of my life, To behold the [a]beauty of the Lord, And to inquire in His temple.”

Swahili Translation:

Mtu wa Mungu uliyeokoka, kaa mbali na UNAJISI na hakikisha unaishi maisha MATAKATIFU ili umfanye Roho wa Bwana akae na wewe. Ili ufurahie maisha ndani ya Kristo, tii maaagizo yanayotoka kwa Mungu.

 Isaya 1:19 “Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi”

Kwenye kufanya kazi ya Mungu, uwe tayari kutumwa bila mjadala, wala usiruhusu maswali akilini mwako.

Isaya 6: 8-9 “Kisha nikaisikia sauti ya Bwana, akisema, Nimtume nani, naye ni nani atakayekwenda kwa ajili yetu? Ndipo niliposema, Mimi hapa, nitume mimi. Naye akaniambia, Enenda, ukawaambie watu hawa, Fulizeni kusikia, lakini msifahamu; fulizeni kutazama, lakini msione".

Kama hauko tayari kutumwa, hutasikia sauti ya Bwana wala hutaona miujiza ya Mungu na kamwe hutaelewa kwa sababu umekuwa mbishi.

Unaweza ukawa unafunga sana lakini hakuna kinachotokea kwenye maisha yako, kwa sababu hufuati maagizo. Fuata maagizo kwa sababu kuna thawabu. Jifunze kuwa na tabia ya upole na ukarimu, wala usiwe na haraka kufanya maamuzi yako. Jifunze namna ya kumsikiliza Roho Mtakatifu.

Hesabu 12: 3Basi huyo mtu, huyo Musa, alikuwa mpole sana zaidi ya wanadamu wote waliokuwa juu ya uso wa nchi”

Watakie watu wengine mambo mazuri wala usilipe kisasi, vilevile ni lazima uchunge na kudhibiti kinywa chako. Jinenee mwenyewe na wengine mazuri.

Mhubiri 6: 6- 7Naam, ajapoishi miaka elfu mara mbili, asijiburudishe kwa mema; je! Wote hawaendi mahali pamoja? Kazi yote ya binadamu ni kwa kinywa chake, Walakini hata hivyo nafsi yake hashibi.”

Tamani kuwa kwenye hema ya Bwana, penye uwepo wa Mungu wakati wote kama alivyofanya Daudi na iwe ni tabia yako.

Zaburi 27:4 Neno Moja nimelitaka kwa Bwana, Nalo ndilo nitakalolitafuta, Nikae nyumbani mwa Bwana Siku zote za maisha yangu, Niutazame uzuri wa Bwana, Na kutafakari hekaluni mwake”

By Servant of God Apostle and Prophet Josephat Elias Mwingira, Efatha Church.

Comments