IN THE COMMUNITY OF BELIEVERS THERE ARE THREE GROUPS



  1. Believers
  2. Followers
  3. Disciples
Are you a believer, follower or disciple? Don’t live in salvation without knowing which group you belong to.

God does not deal with fans in His kingdom. Who are the fans? Are those who move around churches looking for miracles. When Jesus' disciples returned to Jesus with joy, Jesus asked them why they were happy. They told him that today the lame walked, demons had run away and people were healed, Jesus told them “do not rejoice at this, that the spirits submit to you, but rejoice that your names are written in heaven.”

For your name to be written in heaven you must stop being a fan and become a believer, meaning that all you do resembles a believer. How will you know a believer? The bible says “all is possible to those who believe” so there is nothing impossible through his faith. Are you a believer? If you are a believer, what have you done through your faith? If your faith has done nothing, then you have not yet become a believer and you are still a fan because you are still looking for miracles.  

Miracles are not for a believer but for those who don’t believe for them to believe.
When the children of Israel went to the Promised Land in the wilderness they were experiencing miraculous manna and quails from above, but after seeing what God had promised to them, the Promised Land, believed and then the miracles ceased because they now believed.
If you are saved and find yourself getting everything easily and then reach to the point where you are waiting for something to happen as you are used to and it never happens know that you are no longer a person of miracle but a believer,
it means that you have to be a doer for a miracle to happen and not waiting for it.

Swahili Translation:

KATIKA JAMII YA WAAMINIO KUNA MAKUNDI MATATU MAKUBWA:
  1. Waamini
  2. Wafuasi
  3. Wanafunzi
Je! wewe ni Mwamini, Mfuasi au Mwanafunzi? Usiishi katika Wokovu pasipo kujua upo katika kundi gani la Wokovu.

Mungu hashughuliki na mashabiki katika ufalme wake, mashabiki ni wakina nani? Ni wale wanao zunguka makanisani kutafuta miujiza. Wanafunzi wa Yesu waliporudi kwa Yesu wakiwa na shangwe Yesu akawauliza kwa nini mnafuraha? Wakamwambia leo viwete wametembea, mapepo yamekimbia watu wameponyeka, Yesu akawaambia "msifurahi kwa vile pepo wanavyowatii; bali furahini kwa sababu majina yenu yameandikwa mbinguni".

Ili jina lako liandikwe Mbinguni ni pale ambapo utakuwa umetoka katika ushabiki na kufikia hatua ya kuamini, yaani kila unachokifanya kinafanana na mwamini, utamjuaje mwamini? Biblia inasema “yote yawezekana kwake yeye aaminiye”, inamaana kwamba hakuna kinacho mshinda kupitia imani yake, je! wewe ni mwamini? Kama ni mwamini umefanya nini kupitia Imani yako? Kama imani yako haijafanya chochote haujafikia kuwa mwamini bali bado ni mshabiki kwa maana hiyo bado unatafuta miujiza.

Miujiza si kwa ajili ya mwamini bali ni kwa ajili ya wasioamini ili wapate kuamini. Wakati wana wa Israel walipokuwa wanakwenda nchi ya ahadi walipokuwa jangwani walikuwa wanapata miujiza ya kushushiwa mana na kwale kutoka juu lakini baada ya kukiona kile walicho ahidiwa na Mungu yaani nchi ya ahadi wakaamini na ndipo miujiza ikakoma maana sasa wameamini. Ukiona umeokoka na ukawa unapata kila kitu kwa urahisi na ikafika mahali ukawa unasubiri jambo Fulani litokee kama ulivyozoea na lisitokee ujue wewe si tena wa miujiza bali ni mwamini, maana yake ni kuwa wewe unatakiwa kuwa mtendaji ili muujiza utokee na si kusubiri muujiza.

By Servant of God Apostle and Prophet Josephat Elias Mwingira, Efatha Church.

Comments