A BELIEVER




In a community of believers there are three groups of people:
  1. Believers
  2. Followers
  3. Disciples
Are you a believer, follower or a disciple? Don’t live in salvation without knowing which group you are.

God does not deal with fans in His Kingdom. Who are the fans? It is those who go around churches in search of miracles. When Jesus' disciples returned to Jesus with joy, Jesus asked them why are you happy? They told him today the lame have walked, the demons have fled and people have been healed. Jesus said to them, "Do not rejoice because the demons are subject to you, but rejoice because your names are written in heaven."

Your name will be written in heaven when you will move from being a fan to a point of believing,
that means everything you do is similar to a believer. How will you know a believer? The Bible says all is possible to the one who believes, meaning that nothing prevails through his faith. Are you a believer? If you are, what have you done through your faith? If your faith has done nothing then you have not become a believer but a fan.

Miracles are not for the believer but for those who don’t believe so they may believe. When the children of Israel went to the Promised Land in the wilderness they were receiving miraculous manna and quails from above, but when they reached the Promised Land they believed and then the miracles ceased because they now believed. When you are saved and see that you are waiting for something to happen as you used to and it never happens know that you are no longer a person of miracles but a believer, it means that you have to be a DOER for the MIRACLE to happen and not to WAIT for a MIRACLE.

Swahili Translation:

Katika jamii ya waaminio kuna makundi matatu makubwa:
  1. Waamini
  2. Wafuasi
  3. Wanafunzi
Je! wewe ni mwamini, mfuasi au mwanafunzi? Usiishi katika Wokovu pasipo kujua upo katika kundi gani la Wokovu.

Mungu hashughuliki na mashabiki katika Ufalme wake, mashabiki ni wakina nani? Ni wale wanao zunguka makanisani kutafuta miujiza. Wanafunzi wa Yesu waliporudi kwa Yesu wakiwa na shangwe Yesu akawauliza kwa nini mnafuraha? Wakamwambia leo viwete wametembea, mapepo yamekimbia watu wameponyeka, Yesu akawaambia "msifurahi kwa vile pepo wanavyowatii; bali furahini kwa sababu majina yenu yameandikwa mbinguni".

Ili jina lako liandikwe Mbinguni ni pale ambapo utakuwa umetoka katika ushabiki na kufikia hatua ya kuamini, yaani kila unachokifanya kinafanana na mwamini, utamjuaje mwamini? Biblia inasema yote yawezekana kwake yeye aaminiye, inamaana kwamba hakuna kinacho mshinda kupitia imani yake, je! wewe ni mwamini? Kama ni mwamini umefanya nini kupitia Imani yako? Kama imani yako haijafanya chochote inamaana haujafikia kuwa mwamini bali bado ni mshabiki.

Miujiza si kwa ajili ya mwamini bali ni kwa ajili ya wasiyo amini ili wapate kuamini. Wakati wana wa Israel walipokuwa wanakwenda nchi ya Ahadi walipokuwa jangwani walikuwa wanapata miujiza ya kushushiwa mana na kware kutoka juu, lakini baada ya kufika nchi ya Ahadi wakaamini na ndipo miujiza ikakoma maana sasa wameamini. Ukiona umeokoka na unasubiri jambo Fulani litokee kama ulivyozoea na lisitokee ujue wewe si tena wa miujiza bali ni mwamini, maana yake ni kuwa wewe unatakiwa kuwa MTENDAJI ili MUUJIZA utokee na si KUSUBIRI MUUJIZA.

©Servant of God Apostle and Prophet Josephat Elias Mwingira, Efatha Church.


Comments