THE LOVE OF GOD




We are created in the image and likeness of God, therefore your wife or husband resembles God. If you want to see God look at your wife or your husband, and anything you do to him or her you are doing it to God.

The day a young man says to a lady I love you, it means he is telling God that I love you, and when the lady accept she is also telling God that I love you too. When they are both in Marriage and Rejoicing it means they are enjoying God.

Many people are poor because they want to see God Himself walking and forget that God is in a person.  When you see someone know that you have seen God, don't do anything wrong to that Person because if you do it means you have wronged God and you will cause the wrath of God in your Life.

Don’t you dare hate or hurt anyone in your Life, don’t you dare ask or give divorce to your husband or wife because doing that is like chasing God away from your life. God hates divorce.

Swahili Translation:

PENDO LA MUNGU

Tumeumbwa kwa SURA na MFANO wa Mungu hivyo huyo Mke au Mume wako anafanana na Mungu, unapotaka kumuona Mungu mtazame Mkeo au Mumeo, na chochote utakachokifanya kwake ina maana kuwa unamfanyia Mungu.

Siku kijana anaposema kuwa anampenda binti ina maana kuwa anamwambia Mungu ninakupenda, na siku huyo binti alipokubali ina maana kuwa anasema mimi pia Mungu ninakupenda. Wanapokuwa hao wawili katika Ndoa na Kufurahiana ina maana kuwa wanamfurahia Mungu.

Watu wengi wanakuwa maskini kwa sababu wanataka kumuona Mungu mwenyewe akitembea, wanasahau kuwa Mungu yupo ndani ya Mtu, unapomuona Mtu jua kuwa umemuona Mungu usifanye kitu chochote kibaya kwa huyo Mtu kwa sababu ukifanya hivyo ina maana umemfanyia Mungu na utasababisha hasira ya Mungu kuwaka katika Maisha yako.

Usithubutu kumchukia au kumuumiza Mtu yeyote yule katika Maisha yako, usithubutu kuomba au kutoa talaka kwa Mume au Mke wako kwa sababu ukifanya hivyo inakuwa ni sawa na unamfukuza Mungu katika maisha yako, Mungu anachukia talaka.

©Servant of God Presiding Apostle Josephat Elias Mwingira, Efatha Church.


Comments