LOSING SIGHT




The human being who was created by God and placed at the Garden of Eden lost the grace to see like God because of sin. After being deceived by the devil he disobeyed God’s instructions.

Spiritual blindness occurs to a person after being separated from the Perfection of God. Human dignity went wrong because of the seduction and influence of Satan, which caused them to eat the forbidden fruit.

The serpent's deception began to attack the woman in the Garden of Eden through Seeing and Hearing then memories and decisions were disrupted and they rebelled against God and the fall of Adam and Eve appeared.

THE RESULTS OF LOSING SIGHT
1. Separation from God’s perfection
From the time the woman was deceived then a spirit of witchcraft and lies entered into them and they wanted to listen to the lie that brings blindness. Genesis 3: 1- 2, 6 -7

2. Separation from your help Sin is a rebellion that has made the world fall into chaos and lead to the difficult conditions we see in the world's society and the great destruction of God's creation. Sin always separates man from God, who is his beginning and help. God is man's help and hope in all things. Psalm 46:1 “God is our refuge and strength, a very present[a] help in trouble.”

3. Losing dream and God’s promises The spirit of sin creates a barrier between man and God, causes a man to lose focus and results in spiritual blindness. Isaiah 59:2Rather, your iniquities have been barriers between you and your God, and your sins have hidden his face from you so that he does not hear.”

Deuteronomy 28:28 "The Lord will afflict you with madness, blindness, and confusion of mind;"
Those are the results of not being ready to do the will of God, so it is best for you to get prepared for your day.

Swahili  Translation:

Mwanadamu aliyeumbwa na kuwekwa kwenye bustani ya Edeni na Mungu, alipoteza Neema ya kuona Kiungu kwa sababu ya kutenda dhambi, baada ya kudanganywa na shetani akakosea maagizo ya Mungu.

Upofu wa roho hutokea kwa mtu baada ya kutengwa na Ukamilifu wa Mungu. Heshima ya mwanadamu iliingia dosari kwa sababu ya hila na ushawishi wa shetani, uliosababisha wale tunda walilokatazwa.

Udanganyifu wa nyoka ulianza kumshambulia mwanamke pale bustani ya Edeni kupitia Kuona na Kusikia, ndipo kumbukumbu na maamuzi yakavurugika wakamwasi Mungu na anguko la Adamu na Hawa likatokea.

MATOKEO YA KUPOTEZA KUONA.
1. Unatengwa na Ukamilifu wa Mungu
Tokea mwanamke alipodanganyika ndipo roho ya uchawi na uongo iliingia kwao wakapenda kusikiliza uongo unaoleta upofu. Mwanzo 3: 1- 2, 6 -7

2. Unatengwa na Msaada wako
Dhambi ni uasi uliofanya dunia kuingiwa na uharibifu na kusababisha hali ngumu tunayoiona ndani ya jamii ya ulimwengu na maangamizi makubwa kwa uumbaji wa Mungu. Siku zote dhambi humtenga mtu na Mungu, aliye mwanzo na msaada wake. Mungu ndiye Msaada na Tumaini la mwanadamu katika mambo yote. Zaburi 46:1

3. Unapoteza ndoto na yote uliyoahidiwa na Mungu
Roho ya dhambi inatengeneza kiambaza kati ya mtu na Mungu, inasababisha mtu anakosa mwelekeo na matokeo yake anapata upofu wa macho ya rohoni. Isaya 59: 2 "Lakini maovu yenu yamewafarakanisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia."

Kumbukumbu la Torati 28:28 "BWANA atakupiga kwa wazimu, na kwa upofu, na kwa bumbuwazi la moyo"

Hayo ndiyo matokeo ya kutokuwa tayari kufanya Mapenzi ya Mungu, hivyo ni vyema ukajiandaa kukutana na siku yako.

©Servant of God Presiding Apostle Josephat Elias Mwingira, Efatha Church.

Comments