HOW CAN YOU MAKE YOUR LIFE BETTER?




• How can you make your life better by doing things in quality while desiring to please God 
• If you want to blossom in your life, always desire to do well for the Kingdom of God. If you see there is no blossoming it means you are doing wrong. If you see someone doing well know that that person is doing it with the Holy Spirit. But if the person is doing wrong know that the evil spirit from the devil is dwelling on him/ her

When you see someone’s life is blossoming without debt, living in peace and joy don’t envy that person, but change yourself so that that evil spirit may not dwell on you.  

The evil spirit will not leave you until when you decide to hate the devil. Devil is a thief, a liar and his job is to destroy and kill. If you see yourself in debt then know that devil is with you because his job is to lie and he has infected you with lies for you to be like him. Jesus paid for our debt at the cross so that we may not be charged, but I am surprised today to see the saints in so much debt.

How can you go to a shop, buy a new dress while you are in debt? If you are a God’s person you will want first to clean yourself from that debt but if you are of the devil you will desire to add more debt more that those you already have.

How can you go to a saloon and dress up with expensive hair while you are in debt? Which God do you worship? Pay first your debt then do yours. It is better to stay without eating to pay your debt. If God Himself paid for our debt by giving His only son Jesus Christ to die for us, how can you eat fries for ten thousand or more per day while you are in debt? How can you go to a shop and buy something new for you and your family while you are in debt and you don’t know if the person who owes you has eaten or not? How can you take your child to an expensive school for someone else’s money while his/ her children cannot go to school? This is theft just like any other theft.    

God hated debt that’s why He gave His lovely son Jesus Christ to pay for our debt. If you also want to be a child of God for Him to be happy with you, stay away from debt.

Swahili Translation:

• Utaweza kufanya Maisha yako yawe BORA kwa wewe kufanya vitu kwa Ubora huku ukitamani kumpendeza Mungu

• Ukitaka kuchanua katika Maisha yako siku zote tamani kufanya vizuri kwa ajili ya Ufalme wa Mungu, ukiona hakuna kuchanua maana yake unafanya vibaya. Ukimuona mtu anafanya vizuri jua kuwa anafanya na ROHO MTAKATIFU lakini kama anafanya vibaya jua kuwa Roho mbaya ya Yule mwovu ibilisi imemkalia


Ukimuona mtu anaishi Maisha yake kwa kuchanua, hana madeni bali anaishi kwa AMANI na FURAHA, usimuonee wivu bali wewe unapaswa kubadilika ili hiyo roho mbaya isikukalie.

Roho mbaya haiwezi kuondoka kwako mpaka pale utakapoamua kumchukia ibilisi, ibilisi ni mwizi, muongo na kazi yake ni kuchinja na kuua. Ukiona unadaiwa daiwa jua kuwa ibilisi yuko na wewe maana yeye kazi yake ni uongo hivyo kakuambukiza ili ufanane na yeye. Bwana Yesu alilipa deni zetu pale msalabani ili sisi tusidaiwe, lakini leo nashangaa kuona watakatifu wanapenda kudaiwa sana.

Unawezaje ukaenda dukani ukanunua kitenge kipya wakati unadaiwa? Kama wewe ni wa Mungu utataka kujitakasa kwa kuondokana na madeni lakini kama ni wa yule mwovu utatamani kuendelea kuongeza madeni zaidi ya hayo uliyonayo.

Utaendaje saloon ukatengeneza nywele za gharama wakati unadaiwa? Je! ni Mungu yupi unaye mwabudu? Lipa kwanza madeni ya watu ndipo ufanye ya kwako, ni afadhali hata uache kula ili ulipe madeni ya watu. Kama Mungu mwenyewe alitulipia deni zetu kwa kukubali mwanaye wa pekee Yesu Kristo afe ili atulipie deni zetu wewe unawezaje kula chipsi elfu kumi au kumi na tano kwa siku wakati unadaiwa?. Unawezaje kwenda dukani ukanunua kitu kipya kwa ajili yako na familia yako wakati unadaiwa na haujui yule anaye kudai kama amekula au la. Unawezaje ukampeleka mwanao shule ya gharama kwa pesa za mwenzako na yeye mtoto wake wasiende shule, huu ni wizi tu kama wizi mwingine.

Mungu anachukia madeni na ndiyo maana alimtoa mwanaye mpendwa Yesu Kristo ili atulipie deni zetu, kama unataka kuwa Mwana wa Mungu na ili YEYE akufurahie epukana na madeni.

©Servant of God Presiding Apostle Josephat Elias Mwingira, Efatha Church.


Comments