HOW DO YOU IDENTIFYING A FALSE PROPHET?
A false prophet will always give prophecies that are pleasant to hear, but a real prophet tells you the truth no matter how bitter it is. False prophets are jealous while true prophets are not jealous and they bear the truth of God in them.
When God desires to bring destruction to a place, HE always allows Satan who is the master of evil. When God sees that your ways are twisted, you do not regard to HIS directions, and you have an inquisitive ear, God lets the prodigal spirit to follow you. False prophet display themselves.
It came to a time where Ahab sought to fight, and Jehoshaphat told him to seek a Word from God. He accepted but said that there was one who never gave him pleasing prophecies. 400 prophets came and told him to go to war.
Human’s desire pleasant prophesies more than prophecies that correct them. When God sees that you don’t hear the truth, HE looks for people who can lye to you and lead you to destruction.
©Servant of GOD Apostle and Prophet Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.
Translation:

UTAMJUAJE NABII WA UONGO?
Nabii wa uongo mara zote anaeleza vitu vya kukufurahisha na kukupamba lakini yule wa kweli anakuambia ukweli hata kama utakasirika lakini ndio ukweli wa mambo. Pia nabii wa uongo ana wivu ndani, wale wa kweli hawana wivu bali wana Kweli na Haki ya Mungu ndani yao.
Mungu anapoamua kuleta mabaya mahali anamruhusu Shetani mzoefu wa maovu. Kama Mungu akiona njia zako hazijanyooka na unapoelekezwa hutaki kuelewa, una masikio ya utafiti; Mungu anairuhusu roho ya upotevu ikufuate, Manabii wa uongo wanajitokeza.
Imefika mahali Ahabu amedhamiria kwenda kupigana, Jehoshefat Mfalme akamwambia ni vizuri waulize neno kwa BWANA. Akakubali lakini akasema yupo mmoja ambaye kila anapomuuliza hamwambii yanayomfurahisha! Wakaja manabii 400 wote wakamwambia aende vitani.
Kumbe mwanadamu anapenda aambiwe yanayomfurahisha kuliko yanayomkosoa. Mungu akiona hutaki kupata iliyo Kweli, anatafuta walio wazoefu wa kudanganya ili ufurahi ukaangamie.
©Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.

Comments