Unapotembea katika Utaratibu wa Mungu maisha huwa mazuri lakini kinyume na hapo ni mafarakano na huzuni vitawala katika maisha yako, kila kilichokusudiwa na Mungu kina Utaratibu wake hivyo ukitaka shetani asikuonee fuata Utaratibu wa Mungu aliyouweka katika maisha yako.
Mtu asipofuata Utaratibu uliowekwa na Mungu ni rahisi kwenda jehanamu ya moto, Mungu anayafanya hayo yote kwa sababu ANATUJALI na hataki tuwe na huzuni na kilio, hivyo katika maisha yako ya kila siku jitahidi sana kufuata Utaratibu wa Mungu ili uweze kukutana na BARAKA zako ambazo Mungu amekuandalia katika Mwaka huu wa USHINDI.
©Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.

Comments