TOPIC: ACCEPT TO BE PLANTED IN THE HOUSE OF THE LORD
Those planted in the House of the Lord receive the Power of Aid. Once planted, you need to remain where there is the Power of God but not to loiter around.

In Psalm 92:13 “13They are planted in the house of the LORD; they flourish in the courts of our God.” Remember that when moving into a new place, you are starting new. It is just like when a pupil moves from school to school; it is difficult for him/ her to pass in their exams because they are always starting new. Find a church where you can stay so that you can develop SPIRITUALLY and also so that your Brethren my recognize you and learn about your whereabouts. In this way God can reveal HIMSELF to you.

In Psalms 92:14 “They still bear fruit in old age; they are ever full of sap and green,” Those that are planted bear fruits of righteousness and all those following them will get saved. They also live to see the Power of God in their lives, proclaim the Kindness of the Lord and HIS deeds and are ready to bear fruit for HIM and also work together with HIM.

Proverbs 8:17 “I love those who love me, and those who seek me diligently find me.” God works with those who love HIM while HE visits them in work HE gave them and hence giving them HIS Blessings. When you allow yourself to be planted and to bear fruit, you will start to see Prosperity. God will check to see whether you are moving in HIS ways and also despise evil, so that HE can give you HIS Blessings.
©Servant of GOD Apostle and Prophet Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.

Translation:
SOMO: KUBALI KUPANDWA KATIKA NYUMBA YA BWANA.
Waliopandwa katika Nyumba ya BWANA WATAPOKEA NGUVU YA USAIDIZI. Kwa hiyo ukipandwa ni lazima utulie mahali penye Nguvu ya Mungu sio kutangatanga.

Tunasoma;
Zaburi 93:13 “Waliopandwa katika nyumba ya BWANA watasitawi katika nyua za Mungu wetu”.
Kumbuka kila unapoenda mahali papya unaanza upya. Ni kama mwanafunzi anayehama shule kila mara inakuwa vigumu kufaulu mitihani kwani inabidi kila anapokwenda aanze upya. Chagua Kanisa la kutulia ili ukue KIROHO na wenzako wakutambue wewe ni nani unaishi wapi na kadhalika, ndipo Mungu atajifunua kwako.

Tunasoma;
Zaburi 92:14 "Watazaa matunda hadi wakati wa uzee, watajaa utomvu, watakuwa na ubichi”.
Waliopandwa huzaa Matunda ya Haki na husababisha wengi kufikia Wokovu. Hao hudumu na kuziona Nguvu za Mungu katika Maisha yao. Hutangaza Fadhili za Bwana na Matendo yake, wako tayari kumzalia Matunda na kufanya Kazi pamoja Naye.

Tunasoma;
Mithali 8:17 "Nawapenda wale wanipendao, na wale wanitafutao kwa bidii wataniona”.
Mungu hufanya Kazi na wale Wampendao, anapowatembelea na kuwakuta katika Utumishi aliowapa; ndipo huwapa Baraka zake. Ukikubali kupandwa, ukazaa matunda ndipo unaanza kuona Ustawi. Mungu anangalia kama unatembea katika Njia zake na Unachukia uovu ndipo anakupa Baraka zake.
©Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.

Comments