Leviticus 7:12 “For the protection of wisdom is like the protection of money, and the advantage of knowledge is that wisdom preserves the life of him who has it.” Problems concerning shame requires God’s Spirit of Wisdom. The book of Psalms says answer a fool with his own stupidity. The main purpose of shame is to demoralize you and it’s only the Spirit of Wisdom that can withstand it.
The Bible says, “If one lacks God’s Wisdom, let him pray for protection.” When they come to you in malice in order to put you to shame, you will silence them by answering in God’s WISDOM. When they desired to trap Jesus, they used trick questions. (Mark 12:14-16) It is Gods Wisdom that protected Jesus here. You might be undergoing shame and pain and they might also be wanting to destroy you; know that with the protection of the Wisdom of God they will be left saying that it is your lucky day and yet not knowing that it is not by luck but by the Spirit of God. We are not healed by luck nor emerge victorious because of luck but we made worthy and also victors. Seek for the Power of Aid. Hallelujah! 
Psalms 71:5-6 “5 For you, O Lord GOD, are my hope, my trust, O LORD, from my youth. 6 Upon You I have leaned from before my birth; you are He who took me from my mother's womb. My praise is continually of you.” HE is your Aid not only in Old age but also as a Child in birth.

© Servant of GOD Apostle and Prophet Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.

Translation:
Mhubiri 7:12 “Kwa maana Hekima ni ulinzi, kama vile fedha ilivyo ulinzi; na ubora wa Maarifa ni ya kwamba Hekima humhifadhi yeye aliyenayo”.

Shida inayohusu aibu inahitaji Roho wa Hekima ya Mungu ili uweze kuishinda. Ukisoma Zaburi inasema mjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake. Kazi ya aibu ni kukufedhehesha, hivyo ni Roho wa Hekima tu atakayeweza kukabiliana nayo.

Biblia inasema, mtu wa kwenu akikosa Hekima ya Mungu na aombe ili apate kulindwa. Wakikufanyia hila ili wakuaibishe, utatoa jibu la HEKIMA YA Mungu litakalo wanyamazisha. Walipotaka kumshambulia Yesu walimuuliza swali la mtego. Ni vema kumpa Kaisari kodi au la? Akawambia leteni dinari na walipoleta, akawauliza, ina picha ya nani ? Wakajibu ni ya Kaisari. Basi akawaambia, mpeni Kaisari yaliyo yake na ya Mungu mpeni Mungu. Hapa ni Hekima ya Mungu ilimlinda Yesu. Inawezekana unapita kwenye maumivu na aibu imekuandama na wanataka kukuangamiza, hata hivyo ukiwa na Ulinzi wa Hekima, watashindwa na kubaki kusema ni bahati yako, kumbe sio bahati yako bali unastahili maana si kwa ujanja bali ni kwa Roho wa Mungu. Hatuponywi kwa bahati wala hatushindi kwa bahati bali Tunastahili na sisi ni Washindi. Tafuta Nguvu ya Usaidizi. Haleluya! Zaburi ya 71:5-6 “Maana ndiwe taraja langu, ee Bwana MUNGU, tumaini langu tokea ujana wangu, nimekutegemea wewe tangu kuzaliwa, ndiwe uliyenitoa tumboni mwa mama yangu, ninakusifu wewe daima”. Anakuwa Msaada wako sio tu katika Uzee hata ukiwa Mtoto mchanga.
© Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.


Comments