SOMO: IMANI;
Waebrania 11:1 “Basi imani ni kuwa na HAKIKA ya mambo
YATARAJIWAYO, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.” Imani ni nini? Imani ni hakika
ya mambo yatarajiwayo, kile unachokitarajia ndiyo tunaita Imani.
Imani huja kwa kusikia lakini inategemea unasikia nini wewe?
Siyo kila unachokisikia kinataleta imani, bali kwa kusikia Neno la Mungu ndipo
Imani inajengwa.
Tunasikia Neno la Mungu kupitia
kwa watu wanaomjua Mungu, hivyo unaposikia Neno la Mungu kwa umakini na
ukatenda sawa sawa na kile Neno linasema unapata uhakika wa kile ulichokisikia,
hii ndiyo Imani. Watu wengi leo hii wanakwenda Kanisani wanasema wanamwamini
Mungu lakini hawaamini kile wanachokisikia kutoka kwa Watumishi wa Mungu, watu
hawa ni ngumu sana kupata Imani.
Kama unataka kuwa na imani
sikiliza Neno la Mungu kutoka kwa Watumishi wake na utende sawa sawa na Neno
linavyosema.
© Mtume na Nabii Josephat Elias
Mwingira - Efatha Ministry.
Comments
Post a Comment