Katika maisha yako jifunze kuwa mwangalifu na epuka kugombana na aliyebarikiwa na Mungu kwa sababu kila alitendalo linafanikiwa, kama atakukasirikia, Mbinguni wanakukasirikia pia na kama ameumizwa na wewe Mbinguni pia wanaumia, hivyo usije kushangaa baada ya miaka kumi ndiyo hukumu yako inakujia kwa sababu tu ulimgusa aliyebarikiwa na Bwana.
Hakuna aliyemgusa Mbarikiwa wa Bwana akafanikiwa katika Maisha yake, hivyo ili uweze kukutana Baraka zako ambazo Bwana amekuandalia katika Maisha yako jifunze kuwaheshimu waliobarikiwa na Bwana.
:-Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.


Comments