Wana wa Israel ili waifikie nchi ya Ahadi ambayo Mungu aliwaahidi haikuwa rahisi, walikaa jangwani kwa muda wa miaka 40 walipitia vikwazo vya kila aina japo kuwa ulikuwa ni Unabii. Walipo ingia nchi ya Ahadi walikutana na mapambano na vita lakini ulikuwa ni Unabii.
Watu wengi siku hizi hawapendi kujifunza au kusikia Neno la Mungu litakalo wasaidia wao kutenda sawa na Mapenzi Ya Mungu bali wanapenda kusikia Unabii tu, hivyo kuwasababisha kuhangaika huku na kule ili kutafuta Unabii. Unapaswa kujua kuwa Unabii upo ili kukutia moyo na kukuwezesha wewe kusonga mbele lakini si kukupa STAHIKI yako, Imani yako ndiyo itakufanya upokee STAHIKI yako kutoka kwa Mungu, kwa sababu Imani yako itakupa Tumaini la kungoja kile unacho kiamini mpaka kitakapo tokea.
Tamani kujifunza Neno la Mungu litakalo kupa Imani na Tumaini la kungoja kile Mungu amekuahidi na si kusikia Unabii ambao hata ukichelewa kutimia kwako utakusababisha wewe kuhangaika huku na kule.
© Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira - EFATHA MINISTRY.

Comments