SUBJECT: BE REAL
Never make yourself to be different from who you are, but be Real, Honest and Faithful. Acting different from how you are is an outcome of hypocrisy, that makes you portray an image which is different from the real you are. This act makes you to flatter so that you may be loved and receive favor before people. This is a character which does not please God since HE desires you to be just as HE created you.

Be Real, because where you were born is real since you have the blood of those who gave birth unto you and you cannot change yourself. May be you were taught to deny yourself, thus you refused to discern yourself. God does not deal with people who don't know who they are.
© Servant of GOD Apostle and Prophet Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.
SOMO: UWE HALISI.
Siku zote Usijifanye kuwa tofauti na ulivyo, bali uwe Mkweli, Mwadilifu na Mwaminifu. Hali ya kujifanya kinyume na ulivyo inatokana na unafiki na uongo alionao mtu, ili kutoa picha nzuri kuliko alivyo. Hali hii inamfanya ajipendekeze, ili apendwe na kukubalika na watu kinyume na hali halisi. Hii ni tabia ya hila moyoni, ambayo Mungu haitaki, bali anakutaka uwe kama alivyokuumba.

Jitahidi kuwa vile ulivyo. Kwa sababu ulikozaliwa ni halisi maana una damu ya hao waliokuzaa na huwezi kujibadilisha. Inawezekana ulifundishwa kujikataa, ukakataa kujitambua. Mungu hashughuliki na watu ambao hawajitambui.
© Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.

Comments