Ni vizuri ukaelewa namna ya kuwa MWANA halisi wa Mungu, unatakiwa kuishi maisha MATAKATIFU ili wakati wa hukumu usihukumiwe. Ni kweli ulizaliwa katika familia ya wanafiki, wezi, na waongo lakini unapookoka unatakiwa UJIFUNZE NENO la Mungu ili kuondokana na hali hiyo, pasipo kujifunza hizo tabia hazitaondoka kwako.
Jifunze kuwa kiumbe kipya, jifunze KUTAMKA maneno mazuri na kutenda mambo MEMA uwe kama Mungu, ili Ibilisi asikuweke hatiani. Unaweza kufanya uovu katika hali ya kujificha lakini tambua Ibilisi anakuona na Mungu anakuona. Hakikisha unatenda HAKI na kuwa mtu MWEMA mahali popote ulipo na kwa kufanya hivyo utakuwa MSHINDI katika kila ulifanyalo.
 ©Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.

Comments

Popular posts from this blog

Mithali 8:17-21 "Nawapenda wale wanipendao, na wale wanitafutao kwa bidii wataniona. Utajiri na heshima ziko kwangu, Naam, utajiri udumuo, na haki pia. Matunda yangu hupita dhahabu, naam, dhahabu safi, na faida yangu hupita fedha iliyo teule. Natembea katika njia ya haki, katikati ya mapito ya hukumu. Niwarithishe mali wale wanipendao, tena nipate kuzijaza hazina zao." Proverbs 8: 17-21 "I love them that love me; and those that seek me early shall find me. Riches and honour are with me; yea, durable riches and righteousness. My fruit is better than gold, yea, than fine gold; and my revenue than choice silver. I lead in the way of righteousness, in the midst of the paths of judgment: That I may cause those that love me to inherit substance; and I will fill their treasures."