Mungu yupo tayari kukusaidia kwa yote unayohitaji ili kufanikisha Mipango na Ndoto zako. Ataondoa kila kikwazo, kipingamizi, uadui na hali ya kushindwa inayokukalibia ili uweze kutimiza mambo ambayo umeyapanga yatokee katika Mwaka huu wa USHINDI, kwa sababu kufanikiwa kwako ndiyo Furaha ya Mungu.
Kila unapofanikiwa katika Maisha yako unasababisha Ufalme wa Mungu Kuongekezeka, Kustawi na Kuleta UTUKUFU na SIFA kwa Mungu, ndiyo maana anasema “Eleza mambo yako upewe haki yako”, Mafanikio ya Wana wa Mungu ni sehemu ya Haki, Urithi na Imani yao kwa Mungu. Kwahiyo katika Mwaka huu wa USHINDI usikate tamaa, fanyia Kazi Maono yako Ili Mungu aweze kukuwezesha zaidi na zaidi.
©Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.


Comments