IBADA YA MKESHA WA MWAKA
2019.
- BWANA atabadilisha Moyo wako uliyo na
hali ya kushindwa na roho yako iliyo na hali ya kukata tamaa nawe utapewa Roho
na Moyo mpya ili upate KUSHINDA kwa Jina la Bwana kila uendapo. Ezekiel
36:26
"Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama"
"Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama"
- #MWAKA 2019
kutakuwa na hali ya kutiwa Nguvu kutoka JUU, wakati unatiwa Nguvu na Bwana kuna
Mambo matatu yatatokea, ukawe mwaminifu katika kumkumbusha Bwana,usinyamaze
mpaka uone kila unachohitaji kimetimia. Isaya 40:29-31 “Huwapa nguvu wazimiao,
humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo. Hata vijana watazimia na kuchoka, na
wanaume vijana wataanguka; bali wao wamngojeao BWANA watapata nguvu mpya;
watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda
kwa miguu, wala hawatazimia.”
• BWANA atakuvika mbawa za
Tai ili upate kuruka juu kwa haraka UYAFIKIE yale yaliyo JUU maana umechelewa,
BWANA atasababisha UHARAKA katika kwenda kwako na kusababisha ile roho ya Tai
ikujilie ili kuyaendea yale yaliyo mbele yako kwa HARAKA. Kazi ya roho ya Tai
ni Kuhuisha, Kuinua na Kukufanya uende mbele kwa HARAKA.
• Nguvu kutoka JUU,
kupitia hiyo roho ya Tai hapatakuwa na sababu ya kuchelewa na kupoteza muda
tena, Bwana atasababisha kila kitu kufanyika kwa wakati wake, Waefeso 5:16
“Mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu.”
• Bwana atasababisha
USAIDIZI kutoka juu, Isaya 51:21-22 “Basi, kwa sababu ya hayo, ulisikilize neno
hili, ewe uliyeteswa, na kulewa, lakini si kwa mvinyo; BWANA, Bwana wako na
Mungu wako, awateteaye watu wake, asema hivi, Tazama, nimeondoa mkononi
mwako........” Vyote vilivyokuwa vinakuchelewesha HAVINA nafasi juu yako tena,
MWAKA Huu ni MWAKA WA MUUJIZA kwako.
:- Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.
Comments
Post a Comment