IBADA YA MKESHA WA MWAKA MPYA 2019:
#MWAKA 2019 ni MWAKA WA USHINDI 'The YEAR OF VICTORY'.

2019 NI MWAKA WA USHINDI, wewe uliyekuwa unashindwa darasani #HAUTASHINDWA tena, uliyekuwa unashindwa kwenye Ndoa #HAUTASHINDWA tena, uliyekuwa unashindwa na magonjwa #HAUTASHINDWA tena, maana BWANA ameruhusu Afya tele.

#MWAKA HUU 2019 kutakuwa na Mambo #SABA yatakayotokea, kuna wengine yatawatokea yote kulingana na walivyoelewa.
    - #MWAKA huu utakuwa ni Mwaka wa MAREJESHO MAKUU katika Maisha yako, Yoeli 2:25 “Nami nitawarudishia hiyo miaka iliyoliwa na nzige, na parare, na madumadu, na tunutu, jeshi langu kubwa nililotuma kati yenu.”
• Mwaka jana Mwaka wa NGUVU kulikuwa na mambo ambayo yalikuwa ni magumu sana lakini Mungu aliruhusu NGUVU yake itujilie ili Tushinde. Kilichokuvusha Mwaka 2018 ni NGUVU ya Mungu pekee.
• Kwa sababu huu ni #MWAKA wa UREJESHO kutakuwa na UTELE katika Maisha yako, katika Nyumba yako hautahangaika kuhusu CHAKULA.
• Na kwa vile ni #MWAKA wa UREJESHO kutakuwa na MASHANGILIO MAKUU maana Mungu atasababisha UREJESHEWE vile ulivyopoteza.
• #MWAKA Huu ni MWAKA wa PEKEE ni MWAKA WA MAREJESHO, kila iitwapo leo utaona MAREJESHO katika Maisha yako, hata wale Watu ambao walikuwa wanakung’ong’a watarejeshwa, kila Biashara uliyokuwa unaifanya ikawa inakwama kwama inakwenda KUREJESHWA na Bwana.
  
  - #MWAKA huu utakuwa ni MWAKA wa UKOMBOZI WA MILKI; Nyumba za Kupanga hazitakuwa juu yako tena utakuwa na za KWAKO na wewe UTAPANGISHA wengine maana Bwana ATAKUREJESHEA. Obadia 1:17 “Bali katika mlima Sayuni watakuwako wenye kuokoka, nao utakuwa mtakatifu; na nyumba ya Yakobo watamiliki milki zao.”
• #MWAKA huu ni Kipindi chako cha KUMILIKI maana Bwana AMERIDHIA UKOMBOLEWE, Usiogope kuanza KUJENGA kwa sababu hauna fedha anza na tofali moja BWANA atamaliza.

• #MWAKA Huu BWANA ataleta MOTO ili kulamba Adui zako nao watateketea, Mungu atasababisha MOTO Ndani yako ili KULAMBA wale wanaoinuka kinyume chako nao WATATEKETEA.
Inaendelea..................
:- Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.



Comments