IBADA YA MKESHA WA MWAKA 2019.
- #MWAKA huu
hakutakuwa na mateso juu yako maana BWANA atakomesha mateso yako, Nahumu 1:9
“Mnawaza nini juu ya BWANA? Yeye atakomesha kabisa; mateso hayatainuka mara ya
pili.” Kama kuteseka umeteseka vya kutosha mateso hayatainuka tena kwako.
- #MWAKA huu patakuwa na MTIKISIKO wa kushangaza katika
Maisha ya wanadamu ili kuruhusu UTUKUFU wa Mungu kuwafunika wale Wampendao,
Mtikisiko huu utakuwa ni wa kuondoa yale yanayozuia wana wa Mungu wasipokee
Baraka za Mungu.
• MTIKISIKO huu utasababisha MEMA ya Milele yakujilie
wewe Mwana wa Mungu.
• Hagai 2:6 “Kwa maana BWANA wa majeshi asema hivi, Mara
moja tena, ni kitambo kidogo tu, nami nitazitikisa hizo mbingu, na hii nchi, na
bahari, na nchi kavu;” Huu ni WAKATI wako ambao Mungu anaenda kukutikisia yale
yanayokuzuia kwenda mbele, atatikisa ili MATAKATIFU yake yakujilie.
• BWANA atakufanya #RUNGU lake,
Yeremia 51:20 “Wewe u rungu langu na silaha zangu za vita; kwa wewe
nitawavunja-vunja mataifa; na kwa wewe nitaharibu falme;” Neno lako litakuwa na
NGUVU, utakapo litamka LITATENDA kwa adui zako, utakapo tamka neno utasababisha
adui zako Wapigwe.
• Kipindi hiki HAKUNA mchawi atakatiza mbele yako,
kipindi hiki ndicho ambacho utatamka neno juu ya ukoo wako na mizimu na
matambiko yanayo kufuatilia yatakimbia. Matambiko na mizimu inasababisha wewe
usisonge mbele.
- BWANA atabadilisha Moyo wako uliyo na hali ya kushindwa
na roho yako iliyo na hali ya kukata tamaa nawe utapewa roho na moyo mpya ili
upate KUSHINDA kwa Jina la Bwana kila uendapo. Ezekiel 36:26 "Nami
nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo
wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama."
:- Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.
Comments
Post a Comment