IBADA YA KWANZA TAREHE 23/12/2018.
MTUMISHI WA MUNGU MAMA ELIAKUNDA MWINGIRA.
MTUMISHI WA MUNGU MAMA ELIAKUNDA MWINGIRA.
Huu ni Mwaka wa NGUVU na unaishia sasa, tumetembea na Mwaka huu tangu Mwezi wa Kwanza Je! NGUVU YA MUNGU ipo kwako?
NGUVU ni Nini, na ni nani aliyenayo? Ni Mungu mwenyewe, Mungu ni MTAKATIFU hivyo yeyote anayeitaka NGUVU ya Mungu ni lazima awe MTAKATIFU.
NGUVU ya Mungu ndiyo inayo Okoa na kumtoa mtu kutoka katika uovu, NGUVU hii inaweza Kumsamehe mtu, inakupa Kujibaini, Kujitambua na Kujua Mema na mabaya.
Ni kwa kiasi gani hiyo NGUVU ya Mungu imetenda Kazi ndani yako, Inawezekana unaishia kusema tu kuwa huu ni Mwaka wa Nguvu lakini hiyo NGUVU haijatenda jambo lolote katika Maisha yako. NGUVU ya Mungu itakupa Kujua kama kuna Mabadiliko kwako au la.
Comments
Post a Comment