IBADA YA KWANZA TAREHE 23/12/2018 EFATHA MINISTRY MWENGE
MTUMISHI WA MUNGU MAMA ELIAKUNDA MWINGIRA.
Yupo adui anayeifanya NGUVU ya Mungu isikae Ndani yako.
       • Ni TABIA ya mtu husika, Tabia yako inaweza kukimbiza NGUVU ya Mungu Ndani yako, kama Tabia yako haijabadilika; tabia ya kiburi, kujiinua na kutokutaka kubadilika, tabia hzii ni adui mkubwa wa NGUVU ya Mungu.
      • Kiburi, hasira ni maadui wakubwa wa NGUVU ya Mungu.
      • Chuki, hii ni tabia ambayo inafanya NGUVU ya Mungu isikae ndani yako.
      • Masengenyo; tumefika mahali Watakatifu tumezoea tabia hii ya masengenyo, imewabana sana Watakatifu wa Mungu hata kupelekea NGUVU ya Mungu kutokukaa kwao. Kama kweli wewe ni Mwana wa Mungu na unapenda kutunza NGUVU ya Mungu ndani yako epuka Masengenyo, ukiona mwenzako amekosea mwite na umuonye lakini usimseme pembeni maana haitamsaidia.
     • Uongo, magomvi, manung’uniko na tamaa mbaya ni adui wa NGUVU ya Mungu.

Comments