IBADA YA KWANZA TAREHE 23/12/2018 EFATHA MINISTRY MWENGE
MTUMISHI WA MUNGU MAMA ELIAKUNDA MWINGIRA.
Faida za kuwa na Nguvu ya Mungu:
1. Inakupa kutoka mahali kwenda mahali pengine, Mahali pa UTUKUFU.
2. Inakutoa kutoka kuwa mtu wa Kawaida na kukufanya uwe Mtu MKUU.
3. Nguvu hii inakupa KUBADILIKA.
4. Nguvu hii inakufanya unakuwa Mtu wa TOBA, MNYENYEKEVU na Asiye Hesabu mabaya ya wengine.
5. Inakufanya unakuwa Mtu wa MSAMAHA, hausubiri mtu akuombe Msamaha, kwa sababu Unapomsamehe mtu aliyekukosea si kwa faida ya yule unayemsamehe bali ni kwa Faida yako mwenyewe, jifunze KUSAMEHE siyo mpaka uombwe Msamaha.
Jibaini kama kweli unayo NGUVU ya Mungu? Kama ukiona kuwa haya hayapo kwako jua kuwa NGUVU ya Mungu haipo ndani yako.

Comments