IBADA YA KWANZA TAREHE 23/12/2018 EFATHA MINISTRY MWENGE.
MTUMISHI WA MUNGU MAMA ELIAKUNDA MWINGIRA.
JINSI YA KUTUNZA NGUVU YA MUNGU KWA WATAKATIFU;
      • Yakobo 1:22-23 “Lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu. Kwa sababu mtu akiwa ni msikiaji wa neno tu, wala si mtendaji, mtu huyo ni kama mtu anayejiangalia uso wake katika kioo.” Ili uweze kutunza Nguvu ya Mungu kwako ni lazima uwe Msomaji wa NENO la Mungu na utende sawa sawa na NENO linavyosema.
      • Ondoa HASIRA kifuani mwako ili uweze kutenda haki ya Mungu, Yakobo 1:20 “kwa maana hasira ya mwanadamu haiitendi haki ya Mungu.” ukiwa na hasira hautaweza kufanya haki ya Mungu.
      • Ondoa MASHAKA ndani yako maana mwenye mashaka hajakamilika, Yakobo 1:6-8 “Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku......”
Unapokuwa na Mashaka katika jambo lolote ulilosema na Mungu hautalipokea, mwisho wa siku utaishia kusema kuwa hakuna MUNGU, mashaka ni adui wa kupokea BARAKA za Mungu na yale Aliyokuahidi.


Comments

Popular posts from this blog

Mithali 8:17-21 "Nawapenda wale wanipendao, na wale wanitafutao kwa bidii wataniona. Utajiri na heshima ziko kwangu, Naam, utajiri udumuo, na haki pia. Matunda yangu hupita dhahabu, naam, dhahabu safi, na faida yangu hupita fedha iliyo teule. Natembea katika njia ya haki, katikati ya mapito ya hukumu. Niwarithishe mali wale wanipendao, tena nipate kuzijaza hazina zao." Proverbs 8: 17-21 "I love them that love me; and those that seek me early shall find me. Riches and honour are with me; yea, durable riches and righteousness. My fruit is better than gold, yea, than fine gold; and my revenue than choice silver. I lead in the way of righteousness, in the midst of the paths of judgment: That I may cause those that love me to inherit substance; and I will fill their treasures."