IBADA YA KWANZA TAREHE 23/12/2018 EFATHA MINISTRY MWENGE.
MTUMISHI WA MUNGU MAMA ELIAKUNDA MWINGIRA.
MTUMISHI WA MUNGU MAMA ELIAKUNDA MWINGIRA.
HATARI YA TAMAA MBAYA.
Yakobo 1:15 “Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti.” Kuna tamaa mbaya na tamaa nzuri, mfano wa tamaa nzuri ni kama ukiona mwenzako ana mtumikia Mungu unasema na mimi natamani kuwa kama yeye, au unapoona mwenzako amefanikiwa unasema natamani kufanikiwa kama yeye hivyo unaongeza bidii katika utendaji wako na kuwa na shauku na kufika pale alipofika na siku moja utafika.
Lakini tamaa mbaya inakuvuta kufanya mabaya na kuziendea njia za mauti. Ukiona mwenzako amenunua gari zuri unatamani kuliharibu ili mfanane, au ukiona mwenzako amefanikiwa unapeleka habari mbaya ili kumharibia, tamaa mbaya inaambatana na wivu. Unaona watu wamefanikiwa na hujui wamepataje hayo mafanikio kwa sababu ya tamaa mbaya wanakushawishi kwenda kwa waganga ili ufanikiwe na unaishia kuangamia. Tamaa mbaya itakuondolea nguvu ya Mungu.
Comments
Post a Comment