SUBJECT: THE LOVE OF GOD
John 3:16 "For God so loved the world, that he gave his only begotten Son, that whosoever believeth in him should not perish, but have everlasting life."
Whoever that wants to Succeed in life, he/she should first carry the LOVE of God within him/her. LOVE carries lot of things and the first one is GIVING. If you want to succeed at anything, learn to GIVE. If you want a good Marriage, learn to GIVE. Most people want God to do something within their lives but they are not ready to offer themselves unto HIM. You shall never succeed at anything if you will not follow the principle of LOVE.
Which kind of Giving do you need? It is that kind of LOVE that causes you to die for others. Job died and he was still alive because of LOVE; because of that God blessed him and was proud of him. Once you see that temptations are coming do not say that this church has no Anointing but recognize that GOD is testing you since that you are Blossoming.
Do not love GOD because you have something in your hands or because HE has given you something; but LOVE HIM because you are in LOVE with HIM. Also do not LOVE your husband because he has money to give you, but love him because you are in LOVE with him. Do not be in LOVE because of something, once you do that, it is easy for the devil to capture you.
© Servant of GOD Apostle and Prophet Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.


#Translation


SOMO: PENDO LA MUNGU.
Yohana 3:16 “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.” Yeyote anayetaka Kufanikiwa katika Maisha kwanza kabisa ni lazima alibebe PENDO la Mungu NDANI yake.
PENDO linabeba vitu vingi sana ila cha kwanza ni KUTOA, kama unataka kufanikiwa katika chochote kile Jifunze KUTOA. Kama unataka Ndoa njema jifunze KUTOA. Watu walio wengi wanataka Mungu afanye kitu kwa ajili yao lakini wao hawapo tayari Kujitoa kwa ajili ya Mungu. Hutakaa ufanikiwe katika chochote kile kama hutafuata Kanuni ya PENDO.
Ni aina gani ya KUJITOA,? Ni lile PENDO ambalo linasababisha wewe Kufa kwa ajili ya wengine, Ayubu alikufa ilihali anaishi kwa sababu ya PENDO, kwa sababu hiyo Mungu alimbariki na kujivunia YEYE. Unapoona majaribu yanakuja usianze kusema kuwa Kanisa hili halina Upako bali Mungu anakujaribu maana ameona UMESTAWI.
Usimpende Mungu kwa sababu una kitu katika mkono wako au amekupa kitu fulani, MPENDE Mungu kwa sababu uko katika Mapenzi na YEYE, pia usimpende mumeo kwa sababu ana fedha za kukupa bali mpende kwa sababu uko katika MAPENZI na yeye, usiwe katika PENDO kwa sababu ya kitu ukifanya hivyo ibilisi inakuwa ni rahisi kukunasa.

© Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.





Comments