SOMO: SAFARI YA IMANI.
Unapoianza SAFARI YA IMANI hapo ndipo Mungu, watu na ibilisi watakapogundua TABIA yako, kabla hujaianza Safari ni rahisi sana kusifiwa au kujisifu lakini unapoianza hiyo SAFARI hapo ndipo magumu yanapoanza.
• Kabla hujainza SAFARI ya Imani maisha ni rahisi sana, lakini unapoianza SAFARI ya Imani ile njia nyembamba iendayo Uzimani huanza kufanya Kazi na ndipo watu watajua wewe ni nani, kwamba wewe ni mtenda Mema au Maovu.
• Utakapoianza SAFARI ya Imani Mungu atakutazama Je! UNAMUAMINI au la! Watu watagundua Je! upo kwa MUNGU au wanadamu? na ibilisi pia atagundua uko Upande gani.
Mimi kabla sijaanza SAFARI ya Imani nilijua kuwa ninamjua Mungu lakini baada ya kuanza SAFARI nikagundua kuwa simjui hata kidogo, kabla hujaanza SAFARI ya Imani utajidanganya kuwa una Muamini MUNGU na Kumjua, lakini baada ya kuanza SAFARI ndipo utagundua kuwa Haumjui na Unahitaji kujifunza ili Umjue.
© Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.

Comments