SOMO: SAFARI YA IMANI.
Iwe ni Asubuhi, Mchana, Jioni au Usiku Masika au Kiangazi hakikisha Yesu atakapokuja uwe ni Miongoni mwa watu Watakaoondoka naye.
Wana wa Israel walipotoka Misri walikuwa watu wazima wengi na watoto, lakini katika wote hao ni wawili tu waliofanikiwa kuingia katika Nchi ya Ahadi (Kaanani). Unaweza ukakaa katika Kanisa zuri na Mazingira mazuri kama hili, au ni miongoni mwa waanzilishi wa Kanisa, umekaa kwa muda mrefu ukifundishwa Mahubiri mazuri na kujengwa Kiimani. Umekuwa ukishuhudia Miujiza mbali mbali na Shuhuda zinatolewa Mitaani na Madhabahuni, watu wakieleza kile Mungu anafanya kwao lakini yawezekana kabisa usiwe ni kati ya wale watakao uona Uzima wa Milele.
Hili linaweza likawa ni neno gumu sana kwako lakini inategemea ni kwa jinsi gani unaelewa kile unachokisikia, huwezi kuona Uzima wa Milele kwa sababu unalia au kuja Kanisani, japokuwa kuja Kanisani kuna kusaidia wewe Usikie.
Wana wa Israel wakati wanakwenda katika Nchi ya Ahadi walikutana na changamoto ambazo ziliwapelekea wao kufia jangwani. Haijalishi ni jinsi gani ulianza Safari yako ya Wokovu bali ni kwa jinsi gani unakwenda Kuimaliza. Mungu ni wa Ajabu sana anasema anatangaza Mwisho tangu Mwanzo, unapoanza Safari jua Mwisho wako kwanza kabla hujaanza Safari yako maana unapofanya hivyo inakupa Ujasiri wa kutoishia Njiani. Kabla ya Kuoa au Kuolewa mfahamu kwanza yule mtu ambaye unataka kuanza nae Safari ili usije Ukaoa au Kuolewa na mtu ambaye mtaishia njiani (mtu wa Kuacha).
© Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.



Comments