SOMO: SAFARI YA IMANI.
Kusema tu kuwa Bwana yupo pamoja nami haimaanishi kuwa yupo pamoja nawe, hakikisha unakuwa na UHAKIKA kwamba Bwana yupo pamoja na wewe.
1Petro 2:1-4 “Basi, wekeni mbali uovu wote na hila yote, na unafiki na husuda na masingizio yote.” Safari ya Imani itakuonyesha TABIA yako, unapoianza ile Safari ule uhalisia wako utajionyesha kwa sababu katika Safari ya Imani hakuna kujifanya bali kuna UHALISIA.
Mfano;- Ukienda Airport (Uwanja wa ndege) kuna baadhi ya mizigo hauwezi kusafiri nayo haijalishi umeinunua kwa gharama kiasi gani, Unaweza kuamua kuacha kusafiri kwa sababu ya vitu au kuamua kuacha vitu na kusafiri?
Katika safari hiyo wa muhimu siyo wewe bali ni ile ndege; unaposafari uwe makini. Katika Safari ya Imani wa muhimu siyo wewe bali ni Yule anayekubeba ambaye ni ROHO MTAKATIFU. YEYE ndiye atakayekwambia kuwa hiki na kile hakitakiwi katika Safari hii na ndiyo maana Yesu akasema kama mnataka kwenda Mbinguni msimkorofishe ROHO MTAKATIFU.
Je! unataka kwenda Mbinguni?
Kilichowafanya wana wa Israel wasiingie katika Nchi ya Ahadi walibeba vitu ambavyo hawakutakiwa kwenda navyo, vitu gani? Walikuwa na unafiki ndani yao, walikuwa na uongo na mashaka. Je kuna vitu unavibeba unaenda navyo katika hii Safari ya Imani? Acha mara moja kama unataka kwenda Mbinguni.
© Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.

Comments