SOMO: SAFARI YA IMANI.
Mwamini hahukumiwi na Ibilisi bali na Mungu, kama umeokoka na unatandikwa na Ibilisi tatizo siyo Ibilisi maana hana mamlaka ya kukuhukumu, ukitaka kujua hili vizuri soma kitabu cha Ayubu. Baya likikutokea fikiri usiombe mpaka utakapo jua tatizo ni nini. Ukiona Watakatifu wanapitia magumu usiwahukumu maana hujui kwa nini wanapitia hayo.
Usimuhukumu mtu ambaye haujui Mungu ana mpango gani na yeye huenda huyo mtu ndiye atakayekuombea kesho.
1Petro 2:3 “Ikiwa mmeonja ya kwamba Bwana ni mwenye fadhili.” Lazima umuonje Mungu, katika safari ya Imani hapo ndipo unaweza kuonja uzuri wa Mungu lakini nje ya safari ya Imani kamwe hautaweza kuuonja UZURI wa Mungu.
: - Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.

Comments