IBADA YA KWANZA TAREHE 11/11/2018
SOMO: SAFARI YA IMANI.
1 Petro 2:2 “Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu;” Maziwa yasiyo ghoshiwa ni Neno, kwa nini Neno? Kwa sababu Neno linabeba sheria zote za Safari yako ya Imani, Neno ambalo litakujulisha ni kipi cha kubeba au ni kipi cha kuacha; ukiwa nalo utakuwa makini hautakwenda kama unavyotaka bali utakuwa kama Msafiri na kufuata Neno linavyotaka.
Zaburi 1:2 “Bali sheria ya BWANA ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku.” Unapo kuwa katika safari ya Imani hakikisha unatafakari sheria ya Neno, kwa nini? Kwa sababu hautaki kumtia Mungu wivu kwa ajili yako.
Yoshua 1:8 “Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.” Safari ya Imani itakuonyesha TABIA yako wewe ni nani? Je! Unaaminiwa au ni mnafiki?
Kutoka 23:20-21 “Tazama, mimi namtuma malaika aende mbele yako, ili akulinde njiani na kukupeleka mpaka mahali pale nilipokutengezea. Jitunzeni mbele yake, mwisikize sauti yake; wala msimtie kasirani; maana, hatawasamehe makosa yenu; kwa kuwa jina langu limo ndani yake.”
Wakristo wengi wanajikuta wametandikwa na Mungu kwa sababu ya ujinga wao kwani hawafuati maelekezo.
© Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.


Comments