SUBJECT: THE LOVE OF GOD.
John 3:16 "For God so loved the world, that He gave His only begotten Son, that whosoever believeth in Him should not perish, but have everlasting life."

Whoever that wants to succeed in life, first and foremost, must carry the LOVE of God within.

LOVE carries a lot of things and the first is giving. If you want to succeed in anything, learn to give. Most people want God to do things in their lives but they are not ready to offer their lives to God. You will never succeed in anything if you won't follow the principle of LOVE.

Which kind of GIVING? It is that kind of love that is ready to sacrifice for the sake of others. Job died but was still living because of LOVE; because of that God blessed him and was proud of him to the extent the devil envious about him and he wanted to make Job to sin against God; but in all, Job didn't leave his LOVE towards God. Once you see that temptations are coming understand that you are being tested by GOD since HE has seen that you have blossomed.

Do not LOVE God because you are holding something in your hands or because HE has given you something; LOVE God because you are in LOVE with HIM. Also do not LOVE your husband because he has money to give you, but LOVE him because you are in LOVE with him. Do not be in LOVE because of things; once you do that, it is easy to be captured by the devil.
: Servant of GOD Apostle & Prophet Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.


......................................................................................................
#Translation


SOMO: PENDO LA MUNGU.
Yohana 3:16 “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.” Yeyote anayetaka kufanikiwa katika Maisha kwanza kabisa ni lazima alibebe Pendo la Mungu ndani yake.

Pendo linabeba vitu vingi sana ila cha kwanza ni Kutoa, kama unataka kufanikiwa katika chochote kile jifunze Kutoa. Watu walio wengi wanataka Mungu afanye kitu kwa ajili yao lakini wao hawapo tayari Kujitoa kwa ajili ya Mungu. Hutakaa ufanikiwe katika chochote kile kama hutafuata kanuni ya Pendo.

Ni aina gani ya Kujitoa? Ni lile Pendo ambalo linasababisha wewe kuwa tayari kufa kwa ajili ya wengine, Ayubu alikufa ilihali alikuwa anaishi kwa sababu ya Pendo, na kwa sababu hiyo Mungu alimbariki na kujivunia yeye na ndipo ibilisi akaona wivu na kutaka kusababisha Ayubu amkosee Mungu, lakini katika yote Ayubu hakuliacha lile Pendo lake kwa Mungu. Unapoona majaribu yanakuja usianze kusema kuwa Kanisa hili halina Upako bali Mungu anakujaribu maana ameona Umestawi.

Usimpende Mungu kwa sababu una kitu katika mkono wako au amekupa kitu fulani, mpende Mungu kwa sababu uko katika Mapenzi na YEYE, pia usimpende mumeo kwa sababu ana Fedha za kukupa bali mpende kwa sababu uko katika Mapenzi na yeye, usiwe katika Pendo kwa sababu ya Kitu ukifanya hivyo ibilisi inakuwa ni rahisi kukunasa.
© Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.



Comments