Isaiah 43:4 "Since thou wast precious in my sight, thou hast been honourable, and I have loved thee: therefore will I give men for thee, and people for thy life."

Although you are in a painful and sinful situation, but remember that God Loves and Honors you; HE takes you as His precious one. No matter how sinful you are, keep this in your mind that God Loves you, HE honors you because you are so Precious before His sight.

Let these things not depart from your mind; do not think negatively against yourself, think positively. Talk to your heart that you are Loved by your FATHER in Heaven, you are honored by HIM and you are so Precious before His sight; HE created you for His sake and for His Glory.

When you proclaim and decree that, you create a good atmosphere in Heaven for yourself; whoever that is born again is for the Glory of GOD.

© Servant of GOD Apostle and Prophet Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.

........................................................................................................................................

Isaya 43:4 “Kwa kuwa ulikuwa wa thamani machoni pangu, na mwenye kuheshimiwa, nami nimekupenda; kwa sababu hiyo nitatoa watu kwa ajili yako; na kabila za watu kwa ajili ya maisha yako.” Ingawa upo katika hali ya maumivu na dhambi lakini kumbuka Mungu Anakupenda na Kukuheshimu, anakuchukulia wewe kama kitu chake cha Thamani. Hivyo haijalishi una dhambi kiasi gani weka hili katika Akili yako ya kwamba Mungu Anakupenda, Anakuthamini na Kukuheshimu kwa sababu wewe ni wa Thamani machoni pake.

Mambo haya yasiondoke katika akili yako, usijiwazie hasi waza chanya, jisemeshe moyoni mwako kuwa wewe ni mtu UNAYEPENDWA na BABA yako wa Mbinguni, UNAHESHIMIWA na ni wa THAMANI machoni pake, Alikuumba kwa ajili yake na Alikuumba kwa UTUKUFU wake. 

Unapo tangaza na Kukiri hayo unaumba Mazingira mazuri Mbinguni kwa ajili yako, kila aliyezaliwa mara ya pili yaani (aliye okoka) ni kwa ajili ya UTUKUFU wa Mungu.

© Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira – EFATHA MINISTRY.


Comments