The Wealthy get tired in their Minds but are strong in Body. The poor get tired in their Bodies and their Minds become weak; that's why you are so talkative. The Lord JESUS gave an example of the wealth man who gave talents to his three servants. One of them did a huget task that made his body to become tired. He buried the talent that was given to him and did not produce anything; and this is how the sinners are. Always the wrong doers seek to condemn others instead of fulfilling their roles because of the spirit of selfishness. As a person of God, use your Mind and stop complaining.

Ask yourself, "how have you used what was given to you by God", because whatever HE has done unto you, you are able to help another. Others have been healed but have not yet prayed for others who are sick so that they may also be healed. How can God give you the tangible things while you cannot share the spiritual things given unto you? or even keep HIS Purpose! That's why the Lord Jesus says "Hold on what was given unto you" and also "you were freely given so should you" Once we have the Mind of Christ, we shall become WEALTHY; because God gives that HE has accepted; Wisdom and Knowledge so that he/she may be Accomplished. We are supposed to teach others that which we have been commanded so that they may also Teach others. We must work upon that which we have Received, this is when the Joy of what we do shall be manifested.

© APOSTLE & PROPHET JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA (EFATHA MINISTRY).




Watu wenye fedha, huchoka Akili lakini mwili unakuwa na nguvu. Mtu maskini, huchoka Mwili na Akili inakuwa dhaifu, ndio maana anakuwa Muongeaji sana. Bwana Yesu alitoa mfano wa tajiri, aliyetoa talanta kwa watumwa wake watatu. Yule aliyepewa talanta moja, alifanya Kazi kubwa na kuuchosha mwili wake; kwa kuizika hiyo talanta na matokeo yake hakuzalisha kitu; na ndivyo walivyo wenye dhambi. Siku zote, wakosaji wanatafuta Kulaumu wengine kwanza, badala ya kutimiza Wajibu wao maana wana roho ya Wivu na Ubinafsi. Mtu wa Mungu tumia AKILI yako na acha Kulalamika. 

Jiulize umetumiaje ulichotendewa na Mungu, maana chochote alichokufanyia, nawe unaweza kumsaidia mtu mwingine. Watu wengine wameponywa magonwa, lakini hawajamwombea mtu mwingine, ili naye apone. Mungu atakupaje vya mwilini wakati vya rohoni hutaki kugawa, wala kutunza Kusudi lake? Ndio maana Bwana Yesu anasema, shika sana ulichonacho na mmepewa bure toeni bure. Tukiwa na ile nia ya KRISTO, tutakuwa Matajiri wakubwa, maana Mungu humpa yeye aliyemridhia, Hekima na Maarifa, ili afanye KAZI, apate haja ya Moyo wake na ndiko kujaza Hazina yake.Tunatakiwa kuwafundisha watu yale ambayo tumeamriwa ili nao wawafundishe wengine. Tufanyie Kazi hicho tulichokipokea, ndipo furaha ya Kazi inatokea.

© MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA (EFATHA MINISTRY).


Comments