SUBJECT: BEING A PERSON OF REPENTANCE

As a saint, stay away from iniquity and make sure that you live in HOLINESS. 

Daniel 1:8 "But Daniel purposed in his heart that he would not defile himself with the portion of the king's meat, nor with the wine which he drank: therefore he requested of the prince of the eunuchs that he might not defile himself."
Make sure that you have a heart of repentance, a mouth or tongue that confesses and asks for forgiveness. 

Isaiah 6:5 "Then said I, Woe is me! for I am undone; because I am a man of unclean lips, and I dwell in the midst of a people of unclean lips: for mine eyes have seen the King, the Lord of hosts."

When you are guilt, accept and ask for forgiveness so as to cause peace; because you cannot see God without peace. Keeping peace is essential mostly for married couples if you want to shine. Learn to have the habit of meekness and care; don't be in rush to make decisions. Learn how to listen to the Holy Spirit.

Numbers 12:3 "(Now the man Moses was very meek, above all the men which were upon the face of the earth.)"

© APOSTLE & PROPHET JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA - (EFATHA MINISTRY)


SOMO: KUWA MTU WA TOBA

Mtu wa Mungu uliyeokoka, kaa mbali na unajisi na hakikisha unaishi Maisha MATAKATIFU. Danieli 1:8 "Lakini Danieli aliazimu moyoni mwake ya kuwa hatajitia unajisi kwa chakula cha mfalme, wala kwa divai aliyokunywa; basi akamwomba yule mkuu wa matowashi ampe ruhusa asijitie unajisi". Hakikisha unakuwa na MOYO wa Toba, kinywa au ulimi unaokubali makosa na Omba MSAMAHA. Isaya 6:5 "Ndipo niliposema, Ole wangu! Kwa maana nimepotea; kwa sababu mimi ni mtu mwenye midomo michafu, nami ninakaa kati ya watu wenye midomo michafu; na macho yangu yamemwona Mfalme, BWANA wa Majeshi". 

UKIKOSEA, kubali na Uombe msamaha ili kusababisha AMANI, maana huwezi kumuona Mungu bila AMANI. Kutunza Amani ni muhimu sana hasa kwa WANA NDOA kama mnataka Kung’aa. Jifunze kuwa na tabia ya upole na ukarimu, wala usiwe na haraka kufanya Maamuzi yako. Jifunze namna ya kumsikiliza ROHO MTAKATIFU. Hesabu 12: 3 “Basi huyo mtu, huyo Musa, alikuwa mpole sana zaidi ya wanadamu wote waliokuwa juu ya uso wa nchi".

© MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA - (EFATHA MINISTRY).



Comments