SOMO: UPENDO;
Yohana 15:5 “Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.” Kama unataka maisha yako yawe tofauti na mwingine kaa ndani ya Yesu, yaani wewe uwe ndani yake naye awe ndani yako, lakini hii haiwezekani pasipo UPENDO wa Mungu.
Mungu ni PENDO, ukiwa na UPENDO wa Mungu basi tutajua kuwa una Mungu, tutajuaje kuwa una UPENDO wa Mungu? Kwa kuona matendo yako kama yanafanana na mtu mwenye UPENDO au la.
Ili uweze kufanya mambo makubwa na maisha yako yawe ya tofauti na wengine ni lazima ukae ndani ya UPENDO.
© MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA.

Comments