SOMO: TAMKA NENO.

Unapotamka NENO, unasababisha Ulimwengu wa roho KUITIKA usemacho na kuruhusu Dunia kutekeleza. Tamka neno ili kuruhusu ulimwengu wa roho kulichukua na kuelekeza duniani litekelezwe. Ukielewa siri hiyo utaifurahia dunia, kwani vilivyoko vina kazi ya KUTEKELEZA kile roho amesema; kiwe chema au kibaya. 

Pumzi yako ina nguvu ya roho, hivyo chochote utakachosema ni lazima ulimwengu wa roho uitike ili kutekeleza. Ukisema hasi au neno baya kuhusu Maisha au Mazingira yako, shetani huchukua hilo neno na kulifanyia kazi ili kukuletea ubaya.

Ukiona ubaya unakujilia au mazingira mabaya yanayokunyima furaha au kukuondolea Amani, usitamke ile hali mbaya, bali kiri kama NENO linavyosema ili kusababisha hali CHANYA kujitokeza kwenye Maisha yako. Jitahidi kukiri NENO la Mungu wakati wote ili kuruhusu ROHO wa Mungu kulithibitisha upate kupokea Ahadi za Mungu.

: Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira - Efatha Ministry.

Comments

Popular posts from this blog

Mithali 8:17-21 "Nawapenda wale wanipendao, na wale wanitafutao kwa bidii wataniona. Utajiri na heshima ziko kwangu, Naam, utajiri udumuo, na haki pia. Matunda yangu hupita dhahabu, naam, dhahabu safi, na faida yangu hupita fedha iliyo teule. Natembea katika njia ya haki, katikati ya mapito ya hukumu. Niwarithishe mali wale wanipendao, tena nipate kuzijaza hazina zao." Proverbs 8: 17-21 "I love them that love me; and those that seek me early shall find me. Riches and honour are with me; yea, durable riches and righteousness. My fruit is better than gold, yea, than fine gold; and my revenue than choice silver. I lead in the way of righteousness, in the midst of the paths of judgment: That I may cause those that love me to inherit substance; and I will fill their treasures."