SOMO: NGUVU YA MUNGU.
Matendo ya Mitume 1:8 "Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi". Anataka tuwe MASHAHIDI katika Dunia hii, kuanzia hapa tulipo, kule tunakokwenda, tunakofanya Kazi, kwa Majirani zetu na mahali ambapo hatuwezi kufika lakini tunaweza kuwa Mashahidi huko. Tunakuwa Mashahidi wa YESU KRISTO kwa sababu Ushahidi huo ni HABARI NJEMA, nje ya Ushahidi wa YESU KRISTO ni Habari Mbaya.
YESU peke yake ndiye Anayeweza kukupeleka MBINGUNI, KUPONYA magonjwa, KUKUKOMBOA katika umaskini, KUKUSAIDIA Kuishi na Mke kwa Amani maana pasipo YEYE ni vurugu, Ndoa nyingi ni vurugu na kilio kila siku, watoto wanateseka ni kwa sababu hakuna HABARI NJEMA huko ndani. Popote YESU alipo kuna AMANI kwa sababu YEYE ni Mfalme wa Amani, ni MSHAURI Mkuu anaweza kukushauri wapi pa kwenda na nini cha kufanya, anajua jana yako na kesho yako. YESU anajua nini kilitokea ulipozaliwa na kwa nini ulipitia hayo uliyopitia. Mambo mengine yanatokea huelewi kwa nini yanatokea ila YESU Anajua kwa nini yanatokea na ATAKUSAIDIA, YEYE alikuwepo kabla ya uumbaji, kabla hujazaliwa na Ataendelea KUWEPO.
   : Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.



Comments